MAKAMU WA RAIS AWASIRI MWANZA KWA ZIARA
MWANZA
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili
Jijini Mwanza jana jioni na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.
Anthony Mtaka.
Makamu wa Rais anategemewa kuanza ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo kesho mkoani Simiyu.
Katika ziara hiyo
itakayoanza kesho tarehe 19/2/2018 na kumalizika tarehe 22/2/2018,
Makamu wa Rais atakagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Kiloleli
na kuweka jiwe la msingi na baada ya hapo atazungumza na wanachi Lamadi .
Pia Makamu wa Rais ataweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za viongozi wa mkoa katika eneo la Nyaumata.
Miradi mingine ambayo
Makamu wa Rais ataitembelea ni Kukagua Ujenzi wa Barabara za Lami
Bariadi mjini chini ya Programu ya uimarishaji wa Serikali za Mitaa za
Mjini.
Makamu wa Rais
atakagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa la Mwanjoro na kusalimia wananchi
siku ya tarehe 20, pia atasalimia wananchi wa Mwanhuzi Mjini, Mwandoya
(Meatu)
Tarehe 21, Makamu wa
Rais atafungua Kongamano la Elimu ya Juu na Uchumi wa Viwanda Tanzania
kasha atafungua jengo la Utawala la halmashauri ya Itilima na kusalimia
wananchi, kufungua jingo la upasuaji la Samia Suluhu Hassan katika
Hospitali ya Wilaya ya Maswa na kuzungumza na wananchi katika viwanja
vya nguzo nane.
Siku ya tarehe 22, Makamu wa Rais ataongoza Mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria .
TOA MAONI YAKO MATUSI HAPANA....................................
Post a Comment