Header Ads


LESENI ZAWA KIGEZO NA FIMBO YA KUWACHAPIA WACHIMBAJI WADOGO KONDOA

NEWSPAGES_20151012084243
Na Mahmoud Ahmad Kondoa
Pamoja na Afisa madini mkazi kukiri kupokea maombi halali ya wachimbaji wadogo wa madini katika kata ya Changaa wilayani Kondoa Bado haikutosha kutoa maelezo ya kuwapa nafasi ya kuendelea na Ajira yao ya uchimbaji na badala yake mmiliki wa Kidee minning Kupewa nafasi ya kuingia mikataba na wachimbaji hao  kwa kutumia leseni zake kuyatumia mashimo ya wachimbaji na kuwa katika himaya yake kwa shughuli zote za uchimbaji huku wakiyatupilia mbali maombi halali ya leseni ya wachimbaji hao.

Pamoja na suala la ukwepaji kodi za serikali uliofanywa na mwekezaji huyo na kubainika baada ya uchunguzi uliofanywa na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya uliobainishwa kwenye kikao cha 1,12,2017, haikutosha kuwepo kwa mapungufu na suala hilo kutojadiliwa katika kikao hicho jambo ambalo limeleta sintofahamu kwa wachimbaji hao kuona serikali yao imeendelea kuwanyima haki yao ya kimsingi na kumbeba mwekezaji ambaye hakujitosheleza kuwa na sifa ya kutoheshimu mikataba ya ajira,kutoheshimu ajira zao kwa kuwalazimisha kuingia mikataba bila kuangalia kwa undani kiini cha mgogoro huo.

Hayo yamejiri kwenye kikao cha Mkuu wa wilaya Sezaria Makota pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama, Afisa madini mkazi Dodoma,Mkurugenzi wa Kidee Minning (T) ltd na wachimbaji wadogo wa madini kilichofanyika kwenye Ofisi ya kata ya Changaa ambapo wachimbaji hao wanalalamikia hapo awali walikuwa na ajira zao teyari lakini wameshindwa kuheshimiwa na kutakiwa kuburuzwa kisa leseni ambazo hazijainishwa mipaka yake hadi leo.

Tafsiri ya mipaka ya PML mbili No.005012SCZ na No.005013SCZ alizopewa muwekezaji huyo zimekuwa fimbo kali kwa wachimbaji hao ambapo wametakiwa kuendelea kuburuzwa kwa kulazimishwa kuingia mkataba chini ya leseni za mwekezaji japo kumekuwepo na mapungufu kadhaa katika mchakato mzima wa utoaji wa leseni za mwekezaji huyo katika eneo hilo linalobebwa na serikali ya kijiji kwa nguvu kubwa inayopelekea kuzihadaa mamlaka za juu kuaminisha mwekezaji huyo ni mtu salama katika uwekezaji huo.

Leseni hizo ambazo zilitolewa baada ya agizo la mh.Raisi kuzuia utoaji wa Leseni hadi pale itakapoundwa kamisheni ya utaoji wa leseni imekuwa mwiba mkali kwa wachimbaji wadogo wilayani hapa ambapo Kampuni ya Kidee Mining T Ltd inadai wao wamepewa fursa ya kumiliki migodi yote kisheria katika wilaya hiyo kutafiti shughuli za madini ndani ya wilaya hiyo kupitia kwa kamishna wa kanda ya kati Sosthenes Masola 
“Naufunga mgodi huu hadi Tarehe 15 ya mwezi huu ili kuhakikisha usalama na mkataba utaingiwa na wenye mashimo na mwekezaji huyo mwenye leseni Pml 005012SCZ na 005013SCZ na afisa madini hakikisha unashughulikia suala hili mara moja ilikuondoa sintofahamu hii ambayo inaleta taswira mbaya kwenye wilaya yetu”alisema DC Makota

Wakizungumzia Maazimio hayo Mwenyekiti wa mgodi huo Juma Ramadhani Chuha alisema kuwa Alitarajia maamuzi ya yangeheshimu utatuzi wa migogoro kama ilivyokawaida kufika kwenye maeneo yenye mgogoro na kujiridhisha kwa vitendo na angemtaka Afisa wa madini ainishe mipaka ya leseni ili kuondoa sintofahamu ya leseni ambazo zina utata wa mipaka yake kwani zinaingizwa kinyemela kwenye maeneo ya wachimbaji walioomba kihalali na huku kamishna akiwa na kigugumizi hadi leo na lini watapewa majibu ya maombi yao ya leseni katika eneo hilo. 

Kikao hicho kilimalizika na maazimio matano ambayo yalisomwa na Mkuu huyo wa wilaya Sezaria makota yakiwemo kufuta mkataba wa awali waliongia viongozi wa kikundi cha KUMUCHA na mwekezaji bila kuwashirikisha wachimbaji hao, kuingia upya mkataba utakaosimamiwa na idara ya madini mkazi Dodoma na serikali ya wilaya,kuufuta uongozi uliongia mkataba huo,na kuhakiksha mgogoro huo unamalizika ambapo aliwataka wachimbaji kutoenda sehemu yoyote baada ya kikao hicho iwapo watabaini kutotendewa haki na maamuzi yake.

Aidha mkuu huyo wa wilaya aliwataka viongozi wa Kijiji cha Bubu Changaa na mtaa wa tumbelo kuacha kuendesha serikali zao kwa mazoea na badala yake wasimamie misingi ya kisheria katika shughuli zao kwani imeonekana wao ndio chanzo kikubwa cha kuibuka kwa mgogoro huo uliodumu kwa mwaka sasa bila kupatiwa ufumbuzi wa kudumu hadi sasa ambapo wachimbaji baadhi wanadai walikuwa na ajira zao lakini hazikuheshimiwa na kupokwa na mamlaka bila kuangalia athari zake za baadae.

“Unaona kama sisi tulikuwa na misingi ya ajira na tulijiajiri kimsingi katika suala hili na kufuata taratibu zote za kisheria lakini mamlaka inataka tufanye kazi na mwekezaji huyu bila kuangalia suala zima la maombi yetu halali kwenye ofisi za serikali kupata leseni ya kumiliki eneo hilo” alisema Issa Itebeka

1 comment:

  1. Borgata Hotel Casino & Spa Announces Launch of New
    Borgata Hotel Casino & 경산 출장안마 Spa announced the launch of its new 창원 출장마사지 online 양주 출장안마 casino and sportsbook 속초 출장안마 in 대구광역 출장마사지 May. It will open seven days a week

    ReplyDelete

Powered by Blogger.