WANANCHI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA WAMEFANYA MAANDAMANO YA AMANI KUIOMBA SERIKALI KUKAMILISHA MRADI WA MAJI
Rungwe
Wananchi wa Kijiji cha Isyonje Kata
ya Isongole Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya wameiomba Serikali kukamilisha mradi
wa maji uliokwama kwa zaidi ya miaka mitatu wenye thamani ya zaidi ya shilingi
milioni mia tatu.
Wananchi hao wamesema hayo baada ya
kufanya maandamano ya amani wakiandika mabango mpaka kwenye ofisi za kijiji
hicho ya kutaka kukamilika kwa mradi huo ambao umedumu kwa mda mrefu.
Aidha wananchi hao wamesema wanawake
wamekuwa wakitumia mda mwingi kufuata maji umbali mrefu ili kukidhi
mahitaji ya kifamilia na ambapo wamedai kukamilika kwa mradi huo
kutawasaidia kuepuka na magonjwa ya mlipuko.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Asajile
Kamamba amesema yupo sambamba na wananchi kuhitaji kukamilika kwa mradi huo
ambao ulianza kutekelezwa mwaka 2014 mpaka sasa bado haujakamilika.
Muhandisi wa maji wilayani hapo
Bahati Haule amesema kufikia Disemba mwezi huu mkandarasi asipofika eneo la
kazi hawatakuwa tayari kuendelea kufanya kazi na mkandarasi huyo .
Post a Comment