KIM JONG-UN AZURU KIWANDA CHA BIDHAA ZA UREMBO PYONGYANG

Kiongozi wa Korea
Kaskazini Kim Jong-un ametembelea kiwanda ya bidhaa za urembo mjini
Pyongyan akiandamana na mke wake Ri Sol-ju na dada yake Kim Yo-jing.
Vyombo vya habari vilichapisha picha za ziara hiyo siku ya JumapiliKuoneka hadharani kwa Kim Yo-jong, kunakuja muda mfupi baada ya kupandishwa cheo ndani serikali ya Korea Kaskazini.
Bidhaa za urembo kutoka nchi za kigeni zimekuwa adimu nchini Korea Kaskani kutokana na vikwazo.

Licha ya umaarufu wake wa kupigwa picha akiwa katika vituo vya kijeshi na maeneo ya kufanyia majiribio makombora, ziara ya Kim katika kiwanda cha bidhaa za urembo ni moja ya propaganda ya kuhalalisha utawake wake kwa watu wa Korea Kaskazini.

"Licha ya sisi kujua kuwa sio ukweli, ni muhimu kwa utawaka huo kuonyesha watu wake kuwa unaweza kuwapa bidhaa wanazozihitaji,"
Wakati wa ziara hiyo , Kim alikisifu kiwanda hicho kwa kuzalisha bidha za kiwango cha kimataifa, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la KCNA.

Post a Comment