WAKAZI WAISHIO MAMLAKA YA MJI MDOGO WA VWAWA WALALAMIKIA UHABA WA MAJI
Mbozi-songwe
Wakazi
waishio mamlaka ya mji mdogo wa vwawa wilayani mbozi mkoani songwe wamelalamikia
tatizo la uhaba wa maji safi na salama ambalo limedumu kwa muda mrefu na
kuiomba serikali kuwasaidi kutatua tatizo hilo.
Tatizo hilo la maji limekua la muda mrefu ambapo maji
yamekua yakipatikana kwa nadra hata hivyo upatikanaji wake umekua tofauti na
matarajio ya wananchi kwani maji hayo si safi na salama kwa matumizi ya
binadamu.
Mmoja wa wakazi hao merry ernest mkazi wa ilembo amesema kuwa maji yamekua hayafiki kwa wakati
katika bomba zao hali inayopelekea kuyafuata umbali mrefu na kwamba hali hiyo
inawafanya wengi wao kushindwa kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo.
Kwa upande wake antoni sichalwe mkazi wa vwawa
amesema kuwa kutokana na umbali na huo wananchi
wamekuwa wakipata changamoto nyingi
ikiwemo kutekwa na kuporwa mali zao pindi wanapoyafuata maji.
Akizungumzia tatizo hilo mhandisi wa maji wilaya ya
mbozi mkoani hapa AKSON MWANSYANGE licha ya kukiri kuwepo tatizo hilo amesema kuwa uhaba wa maji unasababishwa na
wananchi wenyewe kutokana na baadhi yao kulima karibu na vyanzo vya maji pamoja
na kuchungia mifugo katika vyanzo hivyo.
Mwansyange amesema kuwa juhudi za serikali bado zinaendelea ili
kufikia kiwango kilichowekwa na serikali ambacho ni asilimia 65% ya maji
vijijini.
Post a Comment