MADIWANI KATIKA MANISPAA YA MPANDA WAMPONGEZA RAISI JOHN MAGUFULI KWA KULINDA RASILMALI ZA NCHI
Katavi
MPANDA -KATAVI
Madiwani wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamempongeza rais John Magufuli kwa ujasiri
aliouonesha wa kulinda rasilimali za
nchi hasa katika suala la madini na pia wamelaani vikali
baadhi ya watu wanaobeza jitihada alizozifanya.
Pongezi hizo kwa rais walizitoa jana
kupitia waandishi wa habari ambapo Meya wa Manispaa ya Mpanda Willy Mbogo
alizungumza niaba ya madiwani hao.
Amesema madiwani wa Manipaa ya
Mpanda wameamua kutoa tamko mahsusi la kumpongeza rais Magufuli kwa ujasiri aliouonesha
wa kulinda rasilimali za nchi hasa katika suala zima la madini.
Mbogo alisema wanawalaani vikari
baadhi ya watu ambao wanaobeza jitihada zinazofanywa na
rais za kulinda rasilimali zetu za nchi nahasa
madini kwa ajiri ya manufaa ya Watanzania wote.
Amesema madiwani wa
Manispaa ya Mpanda wanaamini mapato hayo
yatakayopatikana yataongezeka Serikali na halmashauri
zote zitaongeza uwezo wa kuwahudumia wananchi.
Naye diwani wa Kata ya makanyagio
Haidari Sumry aliomba jitihada za rais zisiishie kwenye madini tu
bali nguvu iongezeke kwenye maeneo mengine ili
uchumi wa nchi uweze kukua na
kuongezeka zaidi ya hivi sasa.
Amesema endapo rasilimali za nchi
zitasimamiwa vizuri halmashauri zitanufaika na mapato yataongezeka Serikalini
kwani hata huduma kwenye halmashauri zitaboreshwa
zaidi.
Kwaupande wake diwani wa viti
maalumu katika halmashauri hiyo Getruda Kabinda alisema
kuwa watu ambao walikuwa wakinufaika peke yao na rasilimali za nchi hii ndio
wanaobeza na kupinga jitihada zinazofanywa na rais kwa manufaa ya watanzania
wengi katika kulinda rasilimali za nchi.
Amemuomba rais Magufuli kukaza uzi
kwani watanzania wanyonge wanatambua anachokifanya na kamwe asikatishwe tamaa
na wasaliti wachache kwa maslahi yao,kwani hatua anazochukua japo siku moja
atakufa lakini atabaki anaishi katika mioyo ya wanyonge Kama baba wa taifa
mwalimu Julius Nyerere.
Post a Comment