WATUMISHI WAWILI WA AFYA WAFUKUZWA KAZI NA BARAZA LA MADIWANI MOMBA KWA TUHUMA MBALI MBALI
Momba- SONGWE
MADIWANI katika halmashauri ya wilaya ya Momba mkoani
Songwe,wamewafukuza kazi watumishi wawili ambao ni,Masatu Masisa aliyekuwa
mthamini katika halmashauri hiyo,na Josephi Mbilinyi mhudumu kituo cha afya
Ndalambo,kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za utoro kazini.
Akitoa maamuzi hayo ya
madiwani katika kikao cha baraza la wazi kilichofanyika mwishoni
mwa wiki katika ukumbi wa halmashauri hiyo,makam mwenyekiti wa halmashauri
hiyo,Vedastan Simpasa,amesema wametoa maamuzi hayo baada ya kujiridhisha.
Simpasa ambaye pia ni diwani wa kata
ya Kapele,amesema Mtumishi Masatu Masisa alibainika na kosa la kutokuwepo
kazini kwa muda wa siku 240 pasipo muajiri wake kujua,huku Josephi Mbilinyi
akifanya utoro wa kutokuwepo kazini kwa siku 210 bila taarifa zozote.
Amesema baada ya uchunguzi
kufanyika, muhtasari ulipelekwa kwenye kamati ya fedha na kamati ya maadili
ambao walipendekeza watumishi hao wafukuzwe kazi na muhtasari kupelekwa kwenye
kikao kamili cha wazi cha baraza la madiwani ambao walijigeuza kamati kisha
kutoa maamuzi ya kuwafuta kazi.
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri
hiyo Adrian Jungu,,amesema amepokea maamuzi ya madiwani na kuwa hata yeye baada
ya timu yake kuwachunguza watumishi hao na kutaka watoe utetezi wao ndani ya
siku 14 hawakuweza kufanya hivyo,na kwamba anabariki maamuzi hayo.
Amesema kufukuzwa kwa watumishi
hao,kunafanya idadi ya watumishi waliotimuliwa kuwa 10 kwa mwaka huu na kwamba
kwa sasa watakuwa na uhaba mkubwa wa watumishi,hivyo ataiandikia idara ya
utumishi Tamisemi kuhusu uhitaji wa watumishi wengine watakaoziba nafasi za
watumishi hao.
Post a Comment