WAKULIMA MKOANI RUKWA WAMEIOMBA SERIKALI KUBORESHA MASOKO YA MAZAO YA NAFAKA
KARAMBO-RUKWA
KATIKA jitihada
za kuifikia Tanzania ya
viwanda, wakulima mkoani Rukwa
wameiomba serikali kuboresha masoko
ya mazao ya nafaka sambamba na
kuendana na ushindani wa kibiashara kwa
lengo la kuwawezesha wakulima kuuza
mazao yao kwa bei nzuri na
hatimaye kujikwamua na hali ya kuchumi.
Wakiongea wakati
wa ufunguzi wa maonyesho ya
nanenane yalifanyika katika soko kuu
la mazao ya nafaka wilaya ya kalambo
mkoani Rukwa , wamesema ili kufikia kilimo
chenye tija serikali haina budi
kuleta pembejeo kwa wakati muafaka .
Wamesema
serikali imekuwa ikileta mbolea peke
yake bila mbegu hali ambayo
imekuwa ikiwapa wakati mgumu wakulima
na kushindwa kuzalisha mazao
kwa wingi kutokana na kutumia
mbegu zisizokuwa na ubora.
Aidha wameiomba
serikali kuboresha viwanda vidodogo vya
uzalishaji wa unga wa sembe sambamba
na kutoa elimu elekezi kwa wamiliki
ili kuwawezesha kufungua viwanda vikubwa
zaidi.
Akiongea
kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya
kalambo, katibu tawala wilayani humo Frank
Sichalwe ambae alikuwa mgeni lasimu kwenye ufunguzi
wa maonyesho hayo, amesema lengo ni
kuwawezesha wakulima kubadilishana uzoefu wa kilimo
sambamba na kupata elimu ya
uzalishaji wa mazao.
Post a Comment