UGONJWA WA KIPINDUPINDU WALIPUKA KATIKA KIJIJI CHA SAMAZI WILAYANI KALAMBO MKOANI RUKWA
KALAMBO-RUKWA
UGONJWA wa kipindupindu umelipuka katika kijiji na kata ya Samazi katika Mwambao wa ziwa Tanganyika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa na kusababisha kifo cha mtoto mmoja lina protas miaka 5 na wengine 16 wamelazwa kwenye zahanati ya kijiji hicho.
Akiongea na kituo hiki ofisni kwake afisa tarafa ya Kasanga wilayani humo Peter Mankambila , amesema chanzo cha ugonjwa huo kimetokana na wavuvi waliokuwa wametokea katika kijiji cha Mpasa kilichopo wilaya jilani ya Nkas,ambao walifika kijijini hapo kwa shughuri za uvuvi na kuwambukiza wengine.
Amesema ugonjwa huo uligundulika june 16 ,2017 na kuwa mpaka sasa watu wapatao 16 wamelazwa kwenye zahanati ya kijiji hicho kwa matibabu zaidi .
Afisa afya wilaya humo , Andondile Mwakilima ambae licha ya kukili wazi kuwepo adha hiyo amesema, mpaka sasa watu (8) wameruhusiwa kurudi nyumbani na watu 8 wanaendelea kupatiwa matibabu zaidi na kuwa mpaka sasa wanaendelea kuhamasha jamii kuchimba vyoo vya kudumu kwa lengo la kujiepusha na ugonjwa huo.
Post a Comment