WANANCHI MKOANI SONGWE WAASWA KUTOKUNYWA POMBE KUPINDUKIA ILI KUPUNGUZA VIFOVINAVYOWEZA KUEPUKIKA BAADA YA KUTUMIA DAWA ZA KUFUBAZA VIRUSI VUA UKIMWI
SONGWE
Wakati
serikali ikiendelea na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi Wananchi wa kijiji
cha changombe wilayani songwe mkoani hapa wametakiwa kuacha tabia ya ulevi
wa kupindukia ambao hupelekea baadhi ya
watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kuacha kutumia dawa za kufubaza virusi
hivyo .
Hayo yamesemwa na afisa tarafa ya songwe Godwin
Kaunda wakati wa kilele cha maazimisho
ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika siku ya jana katika kata hiyo ambapo
alikua mgeni rasimi katika maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na ADP wilaya mbozi
mkoani hapa.
Kaunda amesema unywaji wa pombe kupita kiasi hupelekea
wanachi hao kukatisha matumizi ya dawa
za kufubaza virus vya ukimwi hali ambayo inapelekea waathirika wengi wa ugonjwa
huo kudhoofika kiafya na kupoteza maisha kwa harakahali inayopekelekea kupoteza
nguvu kazi ya taifa.
Kwa upande wake Afisa tabibu wa kituo cha afya
Mbuyuni cha wilayani hapo chares mwashambwa amesema endapo mgonjwa akikatisha
dawa basi hali hiyo itapelekea usugu wa dawa hizo na kutokufanya kazi na
matokeao yake ni kudhoofika mwili na kupelekea
kifo.
Mratibu wa
mradi wa uhakika wa chakula kutoka katika shirika la ADP wilaya ya
songwe na Momba Matias Liso amesema wao
kama shirika wanajitahaidi wanahakikisha kila kaya iliyo athirika na ugonjwa
huo inakuwa na uhakika wa chakula ambapo kwa kata hiyo ya chang’ombe kati ya
waliopima virusi vya ukimwi wanaume ni 39 na wanawake 49 huku waliokutwa na
virusi hivyo wakiwa wawili mmoja kati yake ni mwanamke .
Aidha Amesema jamii hutumia muda mwingi kuuguza
wanafamilia waliokutwa na janga hilo na
kwamba wao kama ADP wanajitahidi kuhamasisha jamii kujua afya zao na kufuata
maelekezo wanayopewa na wataalamu.
baadhi ya wananchi waliohudhuria katika maadhimisho
hayo paulina philpo na juma simwita licha kushukuru kwa elimu waliyopewa wameiomba
serikali kutoa elimu kwa jamii husani vijiji ambako ndiko kuna tatito kubwa la
ugonjwa huo kutokana na uhaba wa wataalami ikilinganishwa na mjini.
Post a Comment