EMILY MUGETA ATAKATA KWENYE MECHI YA KUFUZU KOMBE LA UJERUMANI
Mtanzania Emily Mugeta ameanza vyema majukumu yake kwa kuiwezesha klabu yake mpya ya VFB Eppingen kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa kufuzu raundi ya pili kombe la Ujerumani.
VFB Eppingen timu anayochezea Emily Mugeta, wamefanikiwa kufuzu raundi hiyo baada ya kuwang'oa klabu ya TSG Weinheim kwa magoli mawili kwa moja shukrani kwa Niko Grell, Pascal Munzer waliokuwa kwenye kiwango bora kwenye mchezo huo.
VFB Eppingen wanasubiri ratiba ya raundi ya pili kujua mpinzani wake ila kuna nafasi kubwa ya kukutana na klabu za Bundesliga daraja la tatu.
Emily Mugeta amesaini mkataba wa miaka mitatu ya kuitumikia klabu ya VFB Eppingen ya Ujerumani kuanzia msimu ujao wa mwaka 2017/2018, Mtanzania huyo amejiunga na klabu hiyo akitokea klabu ya Sports Freunde Lauffen inayoshiriki madaraja ya chini nchini Ujerumani.
Klabu ya VFB Eppingen inashiriki Ligi ya Verbandsliga nchini Ujerumani, ni Ligi ya nne kwa ukubwa nchini humo baada ya Ligi Kuu ya Ujerumani "Bundesliga", daraja la Pili na la Tatu Bundesliga.
Post a Comment