AFISA ELIMU MKOA WA NJOMBE AKEMEA MAHUSIANO MASHULENI
Mkuu wa wilaya ya njombe Ruth Msafiri |
NJOMBE
AFISA elimu Mkoa wa Njombe amekemea
vitendo vya mahusiano baina ya watoto wa shule na wanafunzi na kusema kuwa
hatakaa kimywa kwa mwalim,u yeyote atakaye bainika kuwa na uhusiano na
mwanafunzi huku akisema kuna waalimu wa kike nnao wameanza tabia hizo.
Afisa huyo anatoa kauli hiyo wakati
wa kufungua mkutano wa Chama cha waalimu Tanzania Kanda ya nyanda za Juu
kusini, Sohitco mkutano ulio jadili changamoto za walimu hapa nchini.
Katibu wa chama cha waalimu anasema
kuwa walimu watambue uhusiano na wanafunzi ni sawa na uhusiano na watoto wao.
Waalimu nao wanakuwa na ushauri kwa
serikali huku wakisema elimu pekee inaweza kupunguza jambo hilo ama kuondoa
kabisa.
Mkuu wa wilaya kila akiwa katika
kusanyiko anazungumza na jamii anayoiongoza juu ya mimba kwa watoto wa shule.
Ili watoto kuwa mbali na mafataki
waalimu wanatakiwa kutoa elimu kwa wanafunzi hao kwa kuwatenga wavulana na
wasichana kila mwalimu kwa jinsia yao kutoa elimu kwa watoto hawa ili kutambua
madhara ya mimba za utotoni na kukatisha elimu zao.
Post a Comment