Header Ads


VIJANA WOTE NCHINI WAMETAKIWA KUWA NA NIDHAMU, UTIIFU, PAMOJA NA ELIMU YA KIMUNGU ILI KUENDANA NA ULIMWENGU WA SASA WA SAYANSI NA TEKNOLOJIA KWANI WENGI WAO HAWANA ELIMU HIYO.


Image result for KANISA LA LAST CHURCH
MBOZI-SONGWE
Hayo yamesemwa na Askofu wa jimbo la mbozi kanisa la Last Church of God Julias Kibona kwenye mkutano wa dini uliofanyika kata ya Ihanda ambapo amesema kuwa baadhi ya Vijana kwa sasa hawana Nidhamu,utiifu,maadili wala Elimu ya kimungu ambapo wao wamejikita zaidi kwenye masuala ya Dunia na kumsahau muumba wao na kuongeza pia hata baadhi ya Viongozi wa Dini wamekuwa na matatiz hayo jambo linalofanya kurudisha nyuma Imani za Waamuni wao kutokana na mafundisho wanayotoa kutokuwa na Ukweli.

Mmoja wa Vijana kanisani hapo Shadrack Kaiga amekiri kuwepo kwa tatizo hilo la baadhi ya Vijana kutomjua mungu na kuwa bize na Shughuli zao na kuahidi kuhamasisha na kutoa Elimu kwa vijana wengine ili kuweza kumrudia Mungu na kuweka Mising imara ya Dini mbalimbali za ndani na Nje ya Nchi.
  
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jimbo la Mbozi Juliasi Mapamba amesema kuwa Vijana wengi hawana ujuzi na Maarifa katika kutoa mafundisho ya dini hivyo inakuwa ngumu kutua huduma hizo sehemu mbalimbali za ndani na nje ya Nchi na kuwataka Vijana kulitilia Mkazo suala hilo

No comments

Powered by Blogger.