LIVERPOOL YAFANIKIWA KUFUDHU HATUA YA MAKUNDI UEFA CHAMPIONS
Wekundu hao wa Anfield waliingia mchezoni wakiwa wanapewa nafasi kubwa kusonga mbele baada ya ushindi wa 2-1 katika mechi ya mguu wa kwanza juma lililopita, na mabao manne zaidi mguu wa pili yaliwawezesha mabingwa hao wa mara tano Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuzu kwa jumla ya mabao 6-3.
Bosi wa Liverpool Jurgen Klopp alitaja kikosi kisichokuwa na mabadiliko kwa kile cha juma lililopita, kwa maana hiyo Mohamed Salah, Dejan Lovren, Trent Alexander-Arnold, Alberto Moreno na Emre Can walikuwepo kufuatia ushindi wa Jumamosi dhidi ya Crystal Palace.
Kwa upande wa Hoffenheim, mchezaji wa zamani wa Leicester City Andrej Kramaric alianza, lakini Sandro Wagner na Serge Gnabry walipata nafasi zao kama kawaida kikosini.
Timu ya nyumbani ilipata nafasi ya kuongoza kipindi cha kwanza ndani ya dakika tatu za mwanzo shuti la Alexander-Arnold lililogonga mwamba lilipotua kichwani mwa Salah, lakini mchezaji huyo aliyetua Anfield akitokea Roma hakuweza kufunga kwani mpira wake ulipaa juu ya goli.
Liverpool walifanikiwa kutikisa nyavu dakika ya 10 baada ya Can kuchukua pasi kutoka kwa Mane.
Dakika nane baadaye Liverpool walifunga bao la pili Salah aliposukuma mpira kwa urahisi kabisa wavuni baada ya Georginio Wijnaldum kugonga mwamba akiwa ndani ya boksi la Hoffenheim.
Liverpool walikuwa na kasi ya ajabu na walifanikiwa kufanya matokeo kuwa 3-0 dakika ya 21 Can alipoweka kimiani bao lake la pili katika mchezo wa usiku wa Jumatano baada ya kupokea pasi kutoka kwa Roberto Firmino.
Hoffenheim walifanya mabadiliko yao ya kwanza dakika ya 24 Mark Uth alipoingia kuchukua nafasi ya kiungo wa zamani wa West Ham United Havard Nordtveit, jambo ambalo lilibadili mfumo wa klabu hiyo ya Bundesliga ambao walionekana kurejea mchezoni.
Wijnaldum alipata nafasi nzuri ya kufunga bao la nne kwa Liverpool dakika ya 55 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Salah, lakini Baumann alifanya kazi nzuri ya kuokoa hatari hiyo kabla ya mlinda mlango wa Hoffenheim kufanya jitihada za kumzuia Mane kufunga dakika mbili baadaye.
Liverpool walipata bao lao la nne dakika ya 63, hata hivyo ni baada ya Jordan Henderson kukimbia hadi eneo la boksi la Hoffenheim kabla ya kupiga pasi mraba kwa Firmino, ambaye naye hakufanya ajizi, alizipasia nyavu na kuiwezesha timu yake kupata bao la nne.
Hoffenheim walifunga bao la pili dakika ya 79 Wagner alipompasia Kramaric na kuweka mpira wavuni, lakini haikutosha, walishachelewa kwani Liverpool walishajihakikishia kupangiwa nafasi kwenye makundi droo ya kesho mchana, itakayofanyika Monaco.
Post a Comment