IMEBAINISHWA KUWA KUTOKUWA NA WALIMU WA KIKE WA KUTOSHA WANAOSOMEA ELIMU KWA WANAFUNZI MAALUMU
NKASI-RUKWA
Imebainishwa kuwa kutokuwa na walimu
wa kike wa kutosha wanaosomea elimu kwa wanafunzi maalumu nimiongoni
mwasababu zinazochangia wanafunzi wa kike wenye ulemavu mkoani Rukwa kuacha
shule nakukosa fursa ya elimu hali inayowafanya wazidi kuwa masikini.
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa
maradi wa kupima uelewa wa kielimu unaojulikana kama international aid service
( IAS) Irene Shayo wakati akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo maalumu cha
kupima uelewa kwa watoto kilichopo Katika wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.
Amesema kuwa kutokana na
kutokuwa na walimu wa kike wa kutosha ambao wanawafundisha wanafunzi
wenyemahitaji maalumu kumekua kukisababisha wanafunzi hao kuacha shule.
Shayo amesema kuwa baadhi ya wanafunzi
wamekuwa wakihudumiwa na walimu wa kiume ambapo wamekuwa wakijidikia vibaya
kwani wanafunzi wa kike wanamaumbile tofauti na wakiume hivyo nibusara
kuhudumiwa na walimu wa kike wanapokuwa na shida.
Amesema kuwa vipo vipindi Katika
makuzi ya mwanadamu ikiwepo ni pamoja na Kupata hedhi sasa wamekuwa hawajisikii
vizuri kuhudumiwa na walimu wa kiume.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa
kutokana na changamoto hizo zimekuwa zikisababisha wanafunzi hao kuacha shule
na kukosa fursa muhimu ya elimu ambayo ingeweza kuwakomboa Katika maisha yao.
Amesema kuwa iwapo kutakuwa
kunawalimu wa kutosha kutasababisha wanafunzi hao kusoma kwa uhuru kwani
wanajua kua iwapo watahitaji msaada walimu hao wapo nawatawasaidia Katika
changamoto zitakazowapata.
Post a Comment