WANANCHI WA KIJIJI CHA ILAMBILA WAGOMA KUFANYA SHUGHURI ZA MAENDELEO WILAYANI KALAMBO MKOA WA RUKWA
KALAMBO-RUKWA
Wananchi
Wa kijiji cha Ilambila
Kata ya Sundu wilaya ya
Kalambo Mkoani Rukwa wamegoma
kujihusisha na shughuli za maendeleo
ikiwemo kuchangia fedha za kuendeshea
mradi wa maji kwa madai ya kuwa
na ukosefu wa uongozi wa kijiji kwa
zaidi ya mwaka mmoja.
Wakiongea
wakati mkutano wa hadhara
uliofanyika kijijini hapo,
wamesema chanzo ni
ukosefu wa uongozi kutia ndani
mwenyekiti wa kijiji na mtendaji na
kuiomba serikali kuingilia kati swala hilo
ikiwemo kufanya uchaguzi mpya.
Hali hiyo
imefanya mbunge wa viti maalumu
mkoani Rukwa Aida Kenani
kuingilia kati mgogoro huo na
kumtaka mtendaji wa kata hiyo
Julis Tete kufanya uchaguzi mapema
ili kufanya shughuri za
maendeleo kuendelea kufanyika kama
ilivyokuwa awali.
Aidha kenani
amewataka wananchi kuacha tabia ya
kuingiza itikadi za vyama kwenye
swala la maendeleo na kusema maendeleo
yanaletwa na wanannchi mwenyewe.
Post a Comment