WADAU WA VIWANDA MKOANI RUKWA WAMEISHAURI SERIKALI YA MKOA WA RUKWA KUTANGAZA BANDARI YA KASANGA
SUMBAWANGA-RUKWA
Katika kuhakikisha Kuwa mkoa wa
Rukwa na taifa Kwaujumla unafanikiwa kupitia Ziwa Tanganyika wadau wa viwanda
mkoani Rukwa wameishauri serikali ya mkoa huo kutangaza bandari ya Kasanga Kuwa
lango la kiuchumi ili nchi inufaike kupitia mataifa yanayotumia Ziwa hilo
Wakizungumza Katika kikao maalumu
kilichowakutanisha wadau wa viwanda kutoka Katika halmashauri za mkoa huo
walisema Kuwa Kwa kupita bandari hiyo mkoa huo na taifa Kwa ujumla utanufaika
iwapo mataifa hayo yataitumia bandari ya Kasanga Kwa kupitishia bidhaa
zao.
Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo Ally
Kasanda alisema Kuwa kuwepo Kwa bandari hiyo ni fursa ambapo mataifa ya
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,Burundi na Zambia yataitumia kupitishia
mizigo yao pindi wanapoipokea Katika bandari ya Dar es salaam.
Alisema Kuwa nchi hizo hazijapakana
na bahari hivyo Kama zikisafirisha mizigo kutoka mataifa ya magharibi kupitia
bahari ya hindi na kuishusha Katika bandari ya Dar es salaam na kisha
kuisafirisha Kwanjia ya nchi kavu mpaka mkoani Rukwa natena kuifikikisha Katika
bandari ya Kasanga kisha kuisafirisha kwanjia ya maji kupitia Ziwa
tanganyika mpaka katika nchini zao.
Kasanda alisema Kuwa iwapo mkoa wa
Rukwa wataiboresha bandari hiyo watafanikiwa na nchi itapata mapato mengi
kwaniwatalipa tozo mbalimbali na kisha wananchi ambao watawekeza Katika sekta
ya viwanda wataweza kusafirisha bidhaa zao Kupitia bandari hiyo na kufanya
biashara ya kimataifa.
Naye Mbunge wa viti maalumu mkoani
Rukwa Bupe Mwakang'ata aliishauri shirika la umemeTanesco,mkoani Rukwa
kuhakikisha linaongeza kasi katika kuwafikishia wananchi wa vijijini umeme ili
nao waweze kunufaika na nia ya serikali Katika kuhakikisha Kuwa wananchi wake
wanamiliki viwanda kwani bila nishati ya uhakika ya umeme suala la
viwanda litakuwa ni hadithi.
Alisema Kuwa wananchi hawanabudi
kunufaika na awamu hii ya tano kwakuwekeza Katika viwanda ili waweze kujikomboa
kiuchumi na kuzalisha ajira ambazo zitawanufaisha wakazi wa mkoa huo.
Kwaupande wake katibu tawala wa mkoa
wa Rukwa Bernard Mkali alisema Kuwa mkoa huo unajumla ya viwanda 950 na alitoa
wito kwawananchi wa mkoa huo kuwekeza zaidi katika viwanda iliwaweze kufungua
fursa ya kiuchumi Kwa wakazi wa mkoa huo.
Post a Comment