WANANCHI TUNDUMA WALIA UKOSEFU WA ENEO LA MAZIKO
TUNDUMA-SONGWE
IMEELEZWA kuwa kukosekana na eneo la
maziko kwa ajili ya kuwasitili wananchi pindi wanapokufa kumeibua sintofahamu
kwa wananchi wa Mji wa Tunduma ambao hawajuhi hatma ya upatikanaji wa eneo
jipya la maziko litakavyopatikana.
Wananchi wa mji wa Tunduma walikuwa
wakizika ndugu zao kwenye eneo la makaburini lililopo kilometa 1 kutoka katika
mji huo lakini eneo hilo limejaa huku baadhi yao wakilazimika kuzika ndugu zao
ndani ya kaburi lingine nakuzuka kwa migogoro isiyokuwa na tija.
Akiuliza katika kipindi cha maswali
ya papo kwa papo,kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika siku za
hivi karibuni,diwani wa kata ya Chipaka,Ayubu Sikagonamo,alisema ni lini
halmashauri itatenga eneo kwa ajili ya maziko baada ya eneo lililokuw
likitumika kujaa?.
Ayubu katika swali hilo,aliongeza
kuwa kumekuwepo na malalamiko na ugonvi mkubwa kwa wananchi kuhusu watu
wanaopoteza ndugu zao kuzika ndani ya kaburi ambalo lina mwili uliozikwa zamani
katika eneo hilo la Kaloleni,na kwamba amekuwa akipokeamalalamiko hayo.
Akijibu swali hilo,kaimu mkurugenzi
wa hakmashauri hiyo,Regina Shashi,alisema ni kweli eneo lile limejaa lakini
halmashauri imetenga eneo la muda lililopo kitongoji cha Mpando kwa ajili ya
kuwasitili watu wanaotangulia mbele za haki huku wakiendelea kutafuta eneo
lingine.
''Mheshimiwa Mwenyekiti,ni kweli
eneo la Kaloleni limejaa,lakini tumetenga eneo la Mpando kwa dharula litumike
kuzikia watu,kipindi hiki tupo kwenye mchakato wa kutafuta eneo jingine kubwa
litakalotumika kwa shughuri za maziko''alisema Shashi.
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa
Tunduma Ally Mwafongo,alisema kutokana na umuhimu wa jambo hilo,alisema
mkurugenzi ni lazima ufanya haraka na uhakikishe eneo jipya la maziko
linapatikana ili kuondoa migogoro na kero zisizokuwa na tija.
Hata hivyo,halmashauri hiyo
imelalamikiwa kushindwa kuwalipa posho wenyeviti wa serikali za mitaa ambapo
madiwani walipitisha malipo ya 50,000/ kati ya hizo 20,000 itumike kulipa pango
la ofisi na 30,000 ni kwa ajili ya posho lakini utekelezwaji bado ni kitendawili,swali
lililoulizwa na diwani wa Tunduma Elode Jivava.
Mkurugenzi Shashi,alisema ni kweli
walipitisha malipo hayo,lakini wameshindwa kulipa kutokana na taratibu za
malipo hazikuwa vizuri na kwamba katika bajeti ijayo malipo ya wenyeviti hao
ambao wanatambua mchango wao wa kujitumakazini yataanza kulipwa.
Post a Comment