HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGWE MKOANI SONGWE,IMETENGA ASILIMIA 80 YA FEDHA ZA MAKUSANYO YA MAPATO
SONGWE-SONGWE
HALMASHAURI ya wilaya ya Songwe
mkoani Songwe,imetenga asilimia 80 ya fedha za makusanyo ya mapato yatokanayo
na ushuru wa pombe za kienyeji kwa ajili ya kuwalipa posho wenyeviti wa vijiji
katika kata ya Ifwenkenya.
Kata ya Ifwenkenya inavyanzo vingi
vya mapato ikiwemo chanzo cha pombe za kienyeji ambazo upikwa kwa wingi
wakitumia mahindi na mtama zikiwa na wateja wengi wa ndani na nje ambapo
halmashauri iliona asilimia 80 ya mapato yaende kwa wenyeviti hao kama motisha,
ili kuwapa moyo wa kufanya kazi.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuibuka
malalamiko kwa wenyeviti hao wakidai kutolipwa posho zao kwa miezi zaidi ya
mitano na kulazimika kupeleka malalamiko yao kwa mkuu wa wilaya ya Songwe
ambapo nakala waliipeleka kwa mwenyekiti wa halmashauri wakitaka kujua sababu
za kutolipwa,
Akizungumza jana kwenye mkutano wa
hadhara,ulioitishwa na mkuu wa wilaya hiyo kwa lengo la kusikiliza matatizo
yanayowakumba wananchi ikiwemo la wenyeviti kutopata stahiki zao kinyume na
makubariano waliojiwekea,kwanyakati tofauti,walitoa kilio chao mbele ya mkutano
huo.
Sarafina Njogoye mmoja wa wenyeviti
katika kata ya Ifwenkenya,alisema kwa muda mrefu kulikuwepo na malalamiko
kuhusu wenyeviti kutopatiwa posho licha ya kuwa wanafanya kazi kubwa hasa ya
kukusanya mapato lakini wanaolipwa mishahara ni maafisa watendaji pekee.
Alisema baada ya kuwepo kwa
malalamiko hayo serikali iliamua kupitia vyanzo vyote vya mapato kwenye kata
hiyo,ambapo waliamua asilimia 80 ya mapato ya pombe za kienyeji ziwe zinatumika
kulipa posho wenyeviti na asilimia 20 iwe inaingia serikalini lakini kwa muda
wa miezi 5 hawajalipwa.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,
Abraham Sambila alisema kutokana na kazi kubwa wanaoifanya wenyeviti wa
vitongoji na vijiji katika kata hiyo,halmashauri iliamua chanzo kimoja cha
pombe za kienyeji mapato yake yatumike kulipa posho wenyeviti ambapo alimuinua
afisa mtendaji wa kata kutoa sababu.
Akijibu sababu hizo,afisa mtendaji
wa kata ya Ifwenkenja Visenti Mpanzu,alisema tatizo la wenyeviti hao kutolipwa
posho imetokana na kutofikia lengo la makusanyo ambapo walikubariana wasaidiane
kukusanya fedha hizo na kuwapa nafasi ya kusimamia makusanyo ambapo hawakufikia
lengo.
Kutokana na majibu hayo,Mwenyekiti
Sambila,alisema hataki kusikia wenyeviti wa vijiji wanahusishwa kukusanya
fedha,na kudai kuwa wamewaajiri maafisa watendaji kukusanya na kusimamia
shughuri zote katika kata zao ikiwemo ya ukusanyaji wa mapato.
Sambila alimueleza afisa huyo mtendaji
wa kata kuwa akiendelea na tabia hiyo,ajiandae kushushwa cheo kuwa afisa
mtendaji wa kijiji,na kwamba kutokana na kazi wanazofanya wenyeviti wa vijiji
ni lazima waheshimiwe.
Post a Comment