WAKAZI WA ILOMBA MKOANI MBEYA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WAO
Wakazi wa ilomba mbeya wakimsikiriza mwenyekiti wa mtaa wao |
ILOMBA-MBEYA
Wananchi wa kata ya
ilomba mkoani mbeya wametakiwa kushirikiana na viongozi wao kuanzia ngazi ya
mtaa kata na hata taifa katika shughuli za maendeleo na kuachana na malumbano
baina yao na viongozi wao.
Hali hiyo imekuja
kutokana na baadhi ya viongozi kushindwa kutatua kero zinazowakabili wananchi
ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero zao hali inayoleta uhasama baina yao
wananchi na viongozi na kupelekea kushindwa kushirikiana kikamilifu katika
shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mtendaji wa kata ya
ilomba jijini mbeya MATIUS NJIZIPYA amesema kuwa bado wanaendelea kuwakumbusha
wananchi juu ya kushiriki shughuli za kimaendeleo kwa kata mitaa hata taifa
ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule na zahanati.
Hata hivyo mtendaji
huyo ameongeza kuwa kutokana na mfumo wa elimu bure wananchi wengi wamekuwa
hawana uelewa wa kutosha juu ya elimu bure pindi wanapohitajika kuchangia fedha
za uboreshaji wa miundo mbinu ya shule kushindwa kutoa kwa wakati na kumwataka wananchi kuwa na uelewa juu ya
elimu bure ili waweze kukamilisha maendeleo yao.
Kwaupande wao wananchi
akiwemo HAMISI JUMA pamoja na AISHA KIMARO wamesema kuwa hali ya kutochangia
fedha za maendeleo ndani ya mitaa na kata zao
ni kutokana na baadhi ya viongozi kutokuwa waaminifu ikiwa ni pamoja na
kutowasomea mapato na matumizi katika mitaa yao.
Post a Comment