WAKAZI WA HEZYA WILAYA YA MBOZI WATAKIWA KUWA NA SUBIRA.
Wakazi wa hezya |
MBOZI-SONGWE
Wananchi katika Kijiji
cha haraka kata ya Hezya Wilayani Mbozi Mkoani Songwe wametakiwa kuwa na Subira
kwa kipindi haki ambacho Serikali inataka kutoa ajira kwa Wahudumu wa Afya
katika Zahanati, Hospitali na Vituo vya Afya nchini kote.
Hayo yamesemwa na
Mganga Mkuu Wilaya ya Mbozi Janeth Makoye baada ya kupoke malalamiko kutoka kwa
Wananchi wa kijiji hicho kukosa wahudumu kwa kipindi cha miaka 16 sasa na
kuwafanya kutembea umbali mrefu kwa
ajili ya kufata huduma hiyo.
Wakizungumza mbele ya
Mbunge wa Vwawa Japhet Hasunga baadhi ya Wananchi hao Anna Chisunga na Mitres
Shale wamesema kuwa katika Zahanati yao hapo kijijini haina Wahadumu jambo
linalowafanya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma za Afya na
wakati mwingine kupoteza ndug zao wanapokuwa njiani
Lamecka Ndabila
mwenyekiti wa kijiji hicho amekiri kuwepo kwa tatizo hilo katika kijiji chake na
kusema kuwa wapo baadhi ya viongozi waliokwisha fika na kuwaahidi wananchi
kuwatekelezea suala hilo lakini mafakinio yoyote yaliyofanyika mpaka sasa na
kuiomba Serikali kuwasaidia katika kutatua adha hiyo.
Kwa upande wake Mbunge
wa Vwawa Japhet Hasunga amesema kuwa suala hilo ni sugu lakini amewahidi
wananchi wa kijiji hicho kufatilia suala hilo kwani nguzo pekee ya mwanandamu
ni Afya na kuongeza kuwa Zahanati bila Wahudumu haiwezi kufanya kazi.
Post a Comment