Buswita ni mchezaji halali wa yanga
Taarifa zilizoibuka sasa zikidai kuwa klabu ya Simba imemuwekea pingamizi kiungo Pius Buswita hazina ukweli wowote kulingana na utafiti mdogo tu tuliofanya.
Kwanza Simba haikuwasilisha malalamiko kuhusu mchezaji huyo kulingana na malalamiko yaliyopokelewa na TFF kutoka timu mbalimbali baada ya dirisha la usajili kufungwa.
Mchezaji pekee wa Yanga ambaye alilalamikiwa ni mlinda lango Youthe Rostand aliyelalamikiwa na African Lyon. Tena naye halalamikiwi kwamba Yanga ilikiuka taratiu za usajili, bali African Lyon inataka ilipwe fidia na Yanga kutokana na usajili wa mchezaji huyo.
Kabla ya kutua Yanga Youthe alikuwa na makataba wa mwaka mmoja na African Lyon hivyo alisajiliwa akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika.
Pili, Buswita hayumo kwenye kikosi cha Simba kilichowasilishwa TFF. Kama alikuwa amesajiliwa na timu hiyo tulitarajia Simba wangewasilisha jina lake TFF.
Tatu, Ni Yanga pekee iliyowasilisha jina la Buswita TFF. Mbao FC imethibitisha kuwa mchezaji huyo amesajiliwa na Yanga na anayo leseni ya kuitumikia Yanga kwenye michuano mbalimbali msimu ujao.
Kuna madai kuwa klabu ya Simba ilimpa pesa Buswita ili asaini katika klabu hiyo lakini Yanga ikawahi kumsainisha.
Hivyo kama Simba inamdai Buswita hilo ni swala lao na mchezaji. Haliwezi kumzuia kuitumikia Yanga kwa kuwa Yanga imemsajili kwa kufuata taratibu zote.
Post a Comment