TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA:MTU MMOJA AMEUAWA NA KUNDI LA WATU WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA KOSA LA WIZI WA KUKU WILAYANI KWIMBA.
KWIMBA-MWANZA
Tarehe 21/08/2017 majira ya 08:45 asubuhi katika kitongoji cha busulwa kata ya ngulla wilaya ya kwimba mkoa wa mwanza, leonard mathias miaka 23, mkazi wa kijiji cha ngulla, aliuawa na kundi la watu waliojichukulia sheria mkononi kwa kupigwa fimbo na mawe sehemu mbalimbali za mwili wake kisha baadae kuchomwa moto hadi kupoteza maisha kwa kosa la wizi wa kuku watano mali ya ester robert, mkazi wa kijiji cha ngulla, kitendo ambacho ni kosa kisheria.
Inasemekana kuwa marehemu aliiba
kuku watano nyumbani kwa bi ester robert kijijini ngulla kisha alikimbilia
kijiji cha jirani cha mwabomba. inadaiwa kuwa wananchi wa kijiji cha
mwabomba walipomuona marehemu akiwa na kuku hao walipata mashaka kisha
walimkamata na baadae walitoa taarifa kijiji cha ngulla ndipo mwenye kuku bi
ester robert alifika na kukabidhiwa kuku wake .
Inadaiwa kuwa baada ya marehemu
kukabidhi kuku kwa mwenye mali, wananchi walimchukua na kwenda nae kituo cha
polisi lakini wakiwa njiani walianza kumshambulia kwa kumpiga fimbo na mawe
sehemu mbalimbali za mwili wake na baadae kumchoma moto. polisi walipata
taarifa kutoka kwa raia wema ndipo walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo na
tukio na kufanikiwa kukamata watu saba ambao wanadaiwa kuhusika kwa namna moja
au nyingine katika mauaji hayo.
Polisi wapo katika upelelezi na
mahojiano watuhumiwa saba waliokamatwa, pindi uchunguzi ukikamilika kisha
ikithibitika watuhumiwa walihusika katika mauaji hayo watafikishwa mahakamani.
aidha upelelezi na msako wa kuwatafuta watu wengine waliohusika kwa namna moja
au nyingine katika mauaji hayo bado unaendelea. mwili wa marehemu tayari
umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza
naibu kamishina wa polisi ahmed msangi anatoa wito kwa wakazi wa jiji na mkoa
wa mwanza akiwataka kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kosa
la jinai, bali pindi wanapomkamata wahalifu au mhalifu wampeleke kwenye kituo
cha polisi ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake. pia
anaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kutoa
taarifa mapema za wahalifu na uhalifu ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye
vyombo vya sheria.
imetolewa
na;
dcp:
ahmed msangi
kamanda
wa polisi (m) mwanza.
Post a Comment