MCHEZAJI WA ZAMANI WA ARSENAL PETIT AMSIFIA KOCHA WAKE WA ZAMANI WA KLABU HIYO MZEE WENGER
London, England.
Emmanuel Petit amesema Kocha Arsene Wenger anapaswa kuthibitisha ubora ubora wake baada ya kupewa majukumu ya kuinoa klabu hiyo kwa miaka mingine miwili.
Malalamiko
makubwa ya mashabiki wa klabu hiyo ni kitendo cha Wenger kutoifanikisha
klabu hiyo kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2017/18.
Petit ambaye ni mfuasi mkubwa wa Arsene, alisema anamheshimu kocha huyo aliyemkuza akitokea akademi ya timu ya vijana ya Monaco kabla ya kuichezea Arsenal.
“Ninatambua kwa nini mashabiki
wanakuwa wakali, najua kwa nini wachezaji walikuwa na hali ya
sintofahamu, hata hivyo naamini Wenger atathibitisha ubora wake msimu
ujao,” alisema Petit
Post a Comment