Header Ads


AMRI YA KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOANI SONGWE YA WARUDISHA MADEREVA BARABARANI




MBOZI-SONGWE
Na manuel kaminyoge
Baadhi  ya madereva hao christofa mwakyusa na fredy kamali wakiongea na kituo hiki mwishoni mwa wiki wamesema wameamua kugoma kwa kushinikiza wenzao waliokamatwa ili waachiwe na kuongeza kuwa wamekuwa wakikamatwa na maaskari hao na kutozwa faini bila risti kitu ambacho kinawapa wasiwasi kuhusu faini hizo .

Daimondi kinyampanda  amesema kuwa hawapo tayari kupeleka gari zao barabarani mpaka wenzao waliokamatwa waachiwe na kuongeza kuwa wapo tayari kukaa muda wowote bila kupeleka magari barabarani.

Mmoja wa wamiliki wa magari hayo maka mahenge amesema kuwa wao kama wamiliki wa magari hayo hawautambui mgomo huo na kumuumba kamanda nyange awape kibali watafute madaleva wengine ili yaendelee kutoa huduma ya usafiri.

 afisa  mfawidhi sumatra mkoa wa songwe Faith ntukamazina  amesema kuwa waliotayari kufanya kazi wafanye na watakao kaidi watachukuliwa sheria kali na kuongeza kuwa wao kama Sumatra hawana taarifa za mgomo huo.

Kwa upande wake kamanada wa jeshi la polisi mkoa wa songwe  matiusi nyange  amesema kuwa yeyote aliyetayari kupeleka gari barabarani apeleke na asiye taka afutiwe reseni yake kwani mgomo wa madreva hao haujafuata taratibu na sheria .
mwishoo.
contact :0762306521 /mwabhulye93@gmail.com


No comments

Powered by Blogger.