KANISA LA FREE PENTECOST CHURCH OF TANZANIA MATAI KATIKA WILAYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA ,LIMETOA MISAADA MBALIMBALI KWA WATOTO YATIMA NA WANAFUNZI
RUKWA-KALAMBO
KATIKA jitihada za
kuongeza kiwango cha elimu mkoani Rukwa , umoja
wa wanawake wa watumishi
(UWW) kupitia makanisa ya
Free Pentecostal church of
Tanzania (F.P.C.T) umetoa misaada
mbalimbali yenye thamani
ya shilingi milioni moja (100,00,00/=)
kwa wanafunzi yatima
na wasio jiweza kwa
lengo la kuwawezesha
kuinua kiwango cha ufauru
kwenye masomo yao.
Hayo yamejili wakati
wa madhimisho ya siku
ya wanawake watumishi (UWW) kupitia
makanisa ya Free pentecost church of
Tanzania na kufanyika katika
kanisa la F.P.C.T
matai katika wilaya
ya kalambo mkoani hapa ,
Awali
akisoma Risala fupi mbele
ya mgeni rasimi
kwenye maadhimisho hayo
Salome Japhet Sota , amesema kwa
kutambua umuhimu wa elimu
kwa taifa la
Tanzania (UWW) inaungana na
Rais wa jamuhuri ya mungano wa
Tanzania John pombe Maghufuli katika kuisapoti elimu hasa
kwa kuwategemiza wanafunzi
ambao ni yatima na wasio jiweza.
Diwani
wa kata ya
Matai Vitus Tenganamba
, ambae alikuwa ni mgeni
rasmi wa maadhimisho
hayo , amewataka wachungani wa madhebu
tofauti kujitokeza kuwasaidia
wanafunzi wasio jiweza
kwa kuwapatia misada mbalimbali ili kuwezesha
kupata elimu bora.
Afisa
elimu ya watu
wazima wilayani humo Njile
Lyebu , amewataka wazazi
na walezi kutambua
umuhimu wa elimu
kwa kuwapeleka watoto wao
shule.
Kwa upande
wake mwangalizi wa
makani hayo wilayani
humo Mchungaji Adrea
Mwakalinga , amesema misaada
hiyo imetolewa kwa wanafunzi wa madehebu
tofauti na kuwa
lengo ni kuwapatia
motisha ya kusoma.
Post a Comment