MKUU WA MKOA WA RUKWA KAMISHNA MSTAAFU ZELOTE STEPHEN AMEKAMATA NA KUZUIA UUZWAJI WA TANI 2,143 ZA MADINI AINA YA “CLINKER”
RUKWA
KATIKA kasi ya kuhakikisha madini ya
watanzania yanawafaidisha watanzania, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu
Zelote Stephen amekamata na kuzuia uuzwaji wa tani 2,143 za madini aina ya
“Clinker” yanayotumika katika kuzalishia saruji kutokana na wingu la
ubabaishaji uliogubika usafirishaji wa madini hayo kwenda nje ya nchi hadi hapo
atakapojiridhisha na utaratibu wa uuzwaji huo.
Sakata hilo limeibuka
baada ya mkuu wa mkoa huo kufanya ziara ya
kushtukiza katika bandari ya Kasanga Iliyopo Wilayani Kalambo mpakani na
nchi ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kupitia Ziwa Tanganyika.
Kupitia
ziara hiyo mkuu wa
mkoa huo zelote Stephen ameshangazwa
na utaratibu wa kuuza udongo
nje ya nchi kwa bei kubwa na
wakati sement inayo zalishwa kupitia
udongo huo inauzwa kwa bei ya
chini.
Usafirishaji wa madini hayo umekuwa
ukifanywa na kampuni ya Mbeya Cement ya jijini Mbeya tangu mwezi Aprili
2017 kuiuzia kampuni ya Burundi Cement ya jijini Bujumbura, ambapo mpaka
mkuu wa mkoa huyo anazuia uuzwaji huo, tayari walikuwa
wameshauza tani 4,760 huku tani moja ikiuzwa kwa dola za kimarekani 128.
Wakati Mh. Zelote akiendelea na ukaguzi
katika bandari hiyo aligundua kuwa kampuni hiyo ya Mbeya Cement ina mzigo
wa tani 2050 za mifuko ya saruji iliyopo bandarini hapo tangu mwezi November
mwaka 2016 na alipoulizwa mwakilishi wa Kampuni hiyo ya Mbeya Sabas Sokoni
amesema kuwa Saruji hiyo imekosa wateja.
Wakati Mh. Zelote akitoa zuio hilo
tayari tani 800 zilikuwa zimo kwenye meli ya MV Tora yenye namba za usajili BY
0064 huku ikiwa na bendera ya Burundi.
Kwa upande wake afisa wa bandari hiyo
Suleiman Kalugendo hakuona tatizo mbali na vibali vya usafirishaji wa madini
hayo kuwa na mashaka.
Post a Comment