WANANCHI WAMTAKA MBUNGE MULUGO, ATIMIZE AHADI YA SOKO ALIYOITOA WAKATI AKIOMBA KURA, MWAKA 2015.
MOMBA-SONGWE
WANANCHI wa kata ya Ifwenkenya
wilayani Momba mkoani Songwe,wamemuomba mkuu wa wilaya hiyo,Samweli Jaremiah
kumkumbusha Mbunge wa jimbo hilo,Philipo Mulugo,(CCM) kutimiza ahadi ya ujenzi
wa soko katika kata hiyo,aliyoitoa wakati akiomba kura ya ubunge mwaka 2015.
Kata ya Ifwenkenya maarufu kwa
shughuri za uchimbaji wa madini ya dhahabu pamoja na kilimo na mifugo huku
idadi ya watu na shughuri za kijamii ikiongezeka siku hadi siku lakini ukosefu
wa soko limekuwa likiathiri shguri za kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo.
Idaya Makweta mfanyabiashara na
mkazi wa Ifwenkenya, alisema mwaka 2015 Mbunge Mulugo alifanya mkutano wa
hadhara na wananchi,ambao walieleza changamoto ya ukosefu wa soko ambapo
wajasiliamali wamekuwa wakitandika bidhaa chini kwa kutandika makaratasi ambapo
mbunge huyo,aliahidikujenga.
Alisema Mbunge huyo aliahidi kujenga
soko hilo kwa gharama zake ili wananchi wa vijiji vilivyopo kwenye kata
hiyo,vipate sehemu sahihi ya kufanyia biashara zao kuliko ilivyo hivi sasa
ambapo wanatandika magunia chini na kupanga bidhaa zao ambazo zinaelemewa na
vumbi hasa kipindi hiki cha masika.
Akipokea maombi hayo ya wananchi
kupitia mkytano huo wa hadhara,mkuu wa wilaya hiyo, Samwel Jeremiah alisema
atamfikishia mbunge Mulugo kama walivyoeleza wananchi hao ambao wanahitaji
kujengewa soko la kiwango cha kati.
Akizungumza kwa njia ya simu,Mbunge
Mulugo,ni kweli aliahidi kujenga soko hilo,wakati akiomba kura na kusema kazi
ya ubunge ni miaka 5 bado anamuda wa miaka 3 kufikia hiyo mitano, katika
kipindi chake cha miaka 2 amejenga masoko 10 katika kata kumi.
Alisema aliposhinda tu ubunge
alianza ujenzi wa soko katika kata ya Magamba,Mbuyuni,Namkukwe na Gua na kata
zingine ambazo idadi yake zipo kumi tayari ujenzi umekamilika na wajasiliamali
wameanza kuuzia bidhaa zao katika masoko hayo na kuwataka wakazi wa Ifwenjenya
wawe watullivu soko litajengwa.
Post a Comment