WALIMU WA FIELD WAKAMATWA NA POLISI KWA KUFANYA MAPENZI NA WANAFUNZI WAO
LUSHOTO-TANGA
Walimu wawili waliokuwa
wakifanya mazoezi kwa vitendo katika shule ya sekondari ya Kikala wilayani
Lushoto mkoani Tanga wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kufanya
mapenzi na wanafunzi wawili wa kidato cha tatu shuleni hapo.
Akizungumza Mkuu wa
Wilaya ya Lushoto ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, January
Lugangika amesema waalimu wa wanafunzi hao wamekikuka maadili ya ualimu na
kwamba watachukuliwa hatua zaidi huku akiongeza kuwa tabia hizo zinaleta
kichefu chefu kwa jamii.
Aidha mwenyekiti huyo
amedai kuwa ushahidi wa tukio hilo umethibitishwa na Daktari ambaye aliwafanyia
vipimo na kuthibitisha ni kweli kitendo hicho kilifanyika
Kwa upande wa Afisa elimu
wa sekondari Wilaya ya Lushoto Kassim Singato amesema endapo kutakuwa na masomo
ya ziada ni lazima yafahamike muda yanapoisha ili wazazi waweze kufuatilia
mwenendo wa watoto wao.
"Inabidi wazazi
muwafatilie watoto wenu kwa kila hatua, mjue wanafanya nini shuleni na kama
mzazi humfatilii anaweza kufanya mambo usiyoyajua na badala yake ukashtukia ana
mimba ya miezi hata sita," alisema Singato.
Post a Comment