BOSI WA SIMBA AWAONYA WAPIGA DILI KLABUNI HAPO
Kuelekea mabadiliko ya kiumfumo wa uongozi ndani ya Klabu ya Simba kumefanya kuwe na mambo mengi yanayoibuka juu ya mchakato huo.
Muhina Kaduguda ambaye ni Katibu Mkuu wa zamani wa Klabu ya Simba amesema kuwa mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo unaweza kuwaathiri wale waliozoea vitu vya dezo.
Kaduguda amezungumza hayo baada ya mkutano wa semina ya mabadiliko ya klabu hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Manyara uliopo ndani ya Viwanja vya Maonyesha ya Sabasaba, Temeke jijini Dar es Salaam.
Amesema ana imani na mchakato wa kuibadili klabu hiyo kutoka kwenye muundo wa zamani na kwenda katika muundo mpya ambao utawafanya wapiga dili kukosa mianya ya upigaji na kujikuta wakiishia kulala njaa.
Post a Comment