HALMASHAURI YA MOMBA YAWAFUTA KAZI WATUMISHI 25 WALIOGHUSHI VYETI.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Momba Mathew Chikoti(kushoto akinyoosha mkono) |
MOMBA-SONGWE
Halmashauri ya wilaya ya Momba
mkoani Songwe,imewafuta kazi watumishi 25 waliobainika kuwa na vyeti bandia
ambapo 17 kutoka idara ya afya, 3, idara ya elimu na 5 kitengo cha utawala.
Akizungumza jana mbele ya kikao cha
baraza la madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya
Momba,Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Mathew Chikoti,alisema kufuatia zoezi la
Rais John Magufuli la kuhakiki watumishi hewa,na wao walifanya hivyo na
kuwakuta 25.
Alisema awali walikuwepo watumishi
hewa na wakaondolewa lakini wakaanza na uhakiki upya na kubaini kuwepo hewa
wengine ambapo baadhi yao walivikimbia vituo vya kazi baada ya kujitambua kuwa
ni feki.
''Kuanzia leo nakuagiza mkurugenzi,watumishi
hawa 25 sio watumishi tena tumewafukuza rasmi,kilichobakia ni kuhakikisha
taratibu za kuwapeleka mahakamani zinafanyika,maana wametumia kodi za wananchi
kudanganya huku wakilipwa mishahara'alisema Chikoti.
Baraza la madiwani momba wakifatiria kwa umakini kwenye kikao |
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri
hiyo,Injinia Maua Mgalla,alisema baada ya uhakiki wa mara ya pili wamebainika
watumishi hao kuwa ni feki,ambapo watatu walibainika kuwa na vyeti vyenye utata
kati ya hao mmoja aliwasilisha cheti chake na wawili walikimbia.
Alisema alisema katika uhakiki huo,
watumishi hewa idara ya afya ni 17,walimu 3 na utawala ni 5 baada ya kubaini
hayo wakapeleka kwa mwenyekiti wa halmashauri ambaye ametangaza rasmi watumishi
hao kufutwa kazi na taratibu za kuwapeleka mahakamani zinafanyika.
Norasto Simbeye,diwani wa kata ya
Mpapa kupitia kikao hicho,alisema watumishi hao wamelipwa fedha za wananchi
kama mshahara wakati wanajua kuwa ni feki hivyo ni lazima wasakwe popote walipo
ili wafikishwe mahakamani kujibu tuhuma zinazo wakabiri.
Hata hivyo,halmashauri ya Momba ni
mpya iliyomegwa kutoka wilaya ya Mbozi ikiwa na changamoto nyingi ikiwemo ya
uhaba wa watumishi hasa wa idara ya afya,ambapo baadhi ya zahanazi zina
muhudumu mmoja na kuwa kuondolewa kwa watumishi hao sekta nyingi zitakumbwa na
uhaba wa watumishi.
Post a Comment