HALMASHAURI YA KYELA YATOA MILIONI 100 KUVIKOPESHA VIKUNDI VYA WANAWAKE NA VIJANA
Halmashauri ya wilaya ya Kyela
mkoani Mbeya,imetoa kiasi cha fedha Milioni 100 kwa ajili ya mikopo kwenye
vikundi 44 vya wanawake na vijana wajasiliamali ili waendeshe shughuri zao huku
ikitenga zaidi ya Milioni 200 kuvikopesha vikundi hivyo,katika bajeti ya mwaka
2017-2018.
Kauli hiyo ilitolewa jana na
mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Dkt,Hunter Mwakifuna kwenye kikao cha baraza la
madiwani kilichokaliwa kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo,huku akitaja
changamoto lukuki zinazopelekea vikundi hivyo kushindwa kurejesha mikopo.
Alisema baadhi ya vikundi vimekuwa
havirejeshi mikopo na vingine vimekuwa vikirejesha nje ya wakati na kuvikosesa
fursa vikundi vingine kupata haki ya kukopa kwa kuwa fedha hizo ni za wote,na
kuwa kutokana na hali hiyo,alisema vikundi vyote vilivyosajiliwa vinatakiwa
kupewa mafunzo.
''Halmashauri ya Kyela imetoa
Mil,100 kuvikopesha vikundi hivyo,na imetenga zaidi ya Mil,200 katika bajeti
ijayo,lakini changamoto iliyopo ni baadhi ya vikundi kushindwa kurejesha mikopo
hatua ambayo inavikosesha fursa vikundi vingine,kwa kuliona hili,lazima
tuvipatie mafunzo''Alisema Dkt,Mwakifuna.
Diwani wa kata ya Ikama Mwl,Zakayo
Mwakagenda,alisema katika kata yake kuna kikundi cha MISE kinachojihusisha na
ujasiliamali wa kusindika mafuta ya mawese lakini halmashauri imeshindwa
kukiwezsha na hata mbio za mwenge zikija zinapitishwa kwenye nkata ambazo
hazina tija.
Alisema ili vijana waweze kunufaika
na rursa za kiuchumi na kufikia uchumi wa kati ni lazima serikali kupitia
halmahauri hiyo, kuviwezesha vikundi hivyo ikiwe ni pamoja na kuvipatia mafunzo
ya ujasiliamali ili viweze kufiki uchumi wa kati.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri
hiyo,Juma Mgatta,alisema alisema hoja za diwani Mwakagenda zinzmashiko,kwa
kushirikiana na wataalam wa sekta ya biashara na uchumi atahakikisha
anakifgikia kikundi hicho na kukiwezesha ha kukiweka kwenye kumbukumbu ili mbio
za mwenge mwakani zinakipitia.
Mgatta alisema awali vikao vilikuwa
vimesimama kutokana na kuzuka kwa mgogoro wa madiwani,na kwakuwa tayari mgogoro
umekwisha alisema watakaa na kujaduli fursa zote za kiuchumi ikiwemo kuvipitia
vikundi vyote na kiviwezesha kisha kuvihamasisha vijisajili kwa vile ambavyo
havitambuliki.
Post a Comment