WAKAZI WA KIJIJI CHA SIKAUNGU WILAYANI SUMBAWANGA MKOANI RUKWA WAMELALAMIKIWA KITENDO CHA ASKARI MAGEREZA WA GEREZA LA MORO WAKIWA NA WAFUNGWA KUWAVAMIA NA KUWATISHIA KWA KUPIGA RISASI
SUMBAWANGA-RUKWA
Tukio hilo lilitokea julai 28 majira ya saa 8 mchana
baada ya wachunga ng'ombe hao kuwa wanachunga katika maeneo ya kijiji chao
ambacho kinapakana na eneo la gereza hilo.
Akizungumza na gazeti hili mwenyekiti wa kijiji hicho
William Khamsini alisema kuwa baadhi ya vijana walikuwa wakichunga ng'ombe wa
familia ndipo waliposhangaa kuona askari magereza wanne wakiwa na wafungwa
wanane wakiwa wamewazunguka na kuanza kuswaga ng'ombe wakidai kuwa wanachungia
katika eneo la gereza hilo.
Baada ya kitendo hicho vijana waliokuwa wamachunga mifugo
hiyo walipiga kelele za kuomba msaada ambapo wananchi wengine walikwenda
kuwasaidia na kisha kuibuka mzozo mkubwa baina ya wananchi hao na askari
magereza pamoja na wafungwa.
Kutokana na hali hiyo askari magereza hao walilazimika
kupiga risasi hewani lakini wananchi hao hawakuogopa mpaka walipofanikiwa
kuondoka na ng'ombe wao na askari polisi hao pia wakiwa na wafungwa waliondoka
zao.
Khamsini alisema kuwa kwa muda mrefu kumekuwepo
Kutoelewana baina ya wananchi hao na watumishi wa gareza hilo ambapo wananchi
wamekuwa wakituhumiwa kuvamia eneo la gereza hilo na kuchungia mifugo yao
kutokana na kijiji hicho kukosa ardhi ya kutosha kwakua eneo kubwa la kijiji
hicho lipo katika shamba la Malonje linalomilikiwa na taasisi na gereza hilo
pamoja na taasisi ya EFATA Ministry ambapo analimiliki kama mwekezaji.
Kutokana na hali hiyo wananchi wa kijiji hicho wamekuwa
wakikutana na changamoto ya kupigwa na kujeruhiwa pindi wanapoingia kuchunga
ama kupita katika upande wa mwekezaji huyo ama upande wa eneo la magereza hali
ambayo mwenyekiti wa kijiji hicho aliiomba serikali ya awamu ya tano
kushughurikia suala hilo kwani limekuwa likisababisha kero kubwa kwa wananchi
hao kwakua hawana eneo maeneo ya kulima, kuchungia mifugo pamoja kujenga nyumba
za kuishi.
Alisema kuwa wameamua kumuandikia barua mkuu wa mkoa wa
Rukwa Zelote Steven ili awasaidie na kama suala hilo ataona liko nje ya uwezo
wake alifikishe kwa raisi aweze kuwatatulia kero zinazowakabili ikiwa ni pamoja
na ukosefu wa ardhi ya kulima na kujenga kwani imekuwa niyamuda mrefu.
Hata hivyo kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa George Kyando
alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema kuwa hawezi kuzungumzia chochote
kwakuwa tukio hilo halijaripotiwa polisi,na alitoa wito kwa wananchi kuwa na
tabia ya kutoa taarifa ya matukio yoyote yanayotokea.
Post a Comment