WAZIRI WA MAMBO YA NDANI NA MBUNGE WA JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI MWIGULU NCHEMBA AMEENDELEA NA ZIARA YAKE MAKETE
TABORA
Waziri
wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu
Nchemba ameendelea na ziara yake ya kutembela kila kijiji katika kila
kata zilizopo jimboni mwake, leo ametembela kijiji cha ujungu kata ya
mekente na kukuta hali ya shule ya msingi ujungu katika kijiji hicho si
nzuri.
Waziri Mwigulu ameshuhudia
ubovu wa madarasa matatu ya shule hiyo yakiwa mabovu kabisa na yenye
nyufa kubwa ambayo ni hatari sana kwa usalama wa wanafunzi huku madarasa
hayo yakiwa hayana sakafu kabisa.
Katika
kupima uwelewa wa wanafunzi wa shule hiyo katika somo la Hisabati
Mheshimiwa waziri Mwigulu aliamua kutoka swali la aljebra ubaoni na
kuita mwanafunzi alijibu, Mwanafunzi mwandu malingumu wa darasa la Sita
aliweza kujibu swali hilo vizuri hali iliyomfurahisha wWaziri Mwigulu na
kumuhaidi akimaliza kufanya mtihani wa darsa la saba na kufauru kidato
cha kwanza atamsomesha.
Post a Comment