WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZAEE NA WATOTO KUTOA AJIRA MIKOA TISA
MPANDA-KATAVI
Wizara ya afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto
inatarajia kutoa ajira kwa watumishi
wa kada mbalimbali za afya a
watakao pewa kipaumbele cha kwanza katika ajira hizo ni wale wakataoomba kufanya kazi katika Mikoa
ya pembezoni ambayo inaupungufu mkubwa
wa watumishi wa Afya.
Kauli hiyo ya
Wizara ya Afya ilitolewa
jana na Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu
wakati alipokuwa akiwahutubia wakazi
wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi
katika uwanja wa mpira
wa Polisi Mpanda alipokuwa akifungua upimaji na utoaji tiba wa magonjwa yasiyo ambukiza.
Waziri Ummy Mwalimu alieleza kuwa Serikali inatarajia kutangaza
ajira za watumishi 52,000
wa kada mbalimbali hivi
karibuni hivyo kwa nafasi
za ajira zitakazo tolewa na
Serikali kwa ajiri ya Wizara yake watatowa kipaumbele
kwa Mikoa tisa ambayo inaupungufu mkubwa wa watumishi wa
Afya.
Alisema kwa wale ambao watakao omba kupangiwa kufanya kazi katika Mkoa wa Dares salaam hawata kuwa na nafasi ya kuchaguliwa kwanza kwani Mkoa huo hauna tatizo kubwa kama ilivyo Mikoa
ya pembezoni .
Aliitaja baadhi
ya Mikoa yenye upungufu mkubwa wa watumishi
wa kada ya
Afya na ambayo itapewa kipaumbele ili kupunguza tatizo la watumishi kwenye
Mikoa hiyo kuwa ni Mikoa
ya Katavi ,Rukwa
,Kigoma, Simiyu, Shinyanga
, Tabora Geita na Kagera.
Waziri Mwalimu pia alieleza kuwa Wizara ya yake imeandaa mpango
wa kupeleka Bungeni mswada wa kumtaka kila
mtu iwe ni lazima kujiunga na mfuko
wa Bima ya afya
Aliwaonya watumishi
wa Wizara hiyo ambao wanatabia
ya kuchezea fedha za kununulia dawa na aliwataka waache mara moja na kwa wle
watakao bainika watachukuliwa hatua kali .
Nae Mkuuwa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga alieleza kuwa
Mkoa wa Katavi unajumla
ya Watumishi 692 kati ya watumishi 2,174
wanaohitajika kati yao 17
ni watumishi wa ngazi ya
Mkoa na 675 ni wangazi
ya Serikali za Mitaa.
Alifafanua kuwa Mkoa wa Katavi unajumla ya upungufu wa watumishi 1,186 sawa na asilimia 69
ya mahitaji ya watumishi.
Kwa mwaka wa fedha wa 2016
na 2017 Mkoa na Halmashauri zake tano umeidhinisha kuajiri jumla
ya watumishi
wapya wa kada mbalimbali za Afya wapatao 422.
Afisa Maendeleo ya Jamii
wa Mkoa
wa Katavi Anna Shumbi alieleza kuwa Mkoa huo ni miongoni mwa Mikoa hapa nchini unaoongoza kwa mimba
za utotoni .
Alieleza sababu zinazochangia Mkoa huo kuwa na mimba nyingi
za utotoni kuwa zimekuwa zikisababishwa na wazazi kuwaacha watoto
wao peke yao bila kuwa na uangalizi hasa kipindi
cha masika ambapo wazazi
uhamia mashambani na kuwaacha watoto peke yao
.
Post a Comment