Klabu ya Ndanda FC imetamba kufanya vyema msimu
ujao wa ligi na kuwataka wadau wa soka nchini kote kusahau yaliyowasibu misimu
mitatu iliyipita ambapo ilishuhudiwa walikua wakihaha kujinusuru kushuka
daraja.
Tambo hizo zimetolewa na mkurugenzi wa ufundi wa
klabu hiyo ya mkoani Mtwara Hamim Mawazo ambaye ameambatana na kikosi cha
Ndanda FC jijini Dar es salaam ambapo kimeweka kambi kwa ajili yakujiandaa na
msimu mpya wa 2017/18.
Hamim ambaye aliwahi kuwa kocha wa kikosi cha
Ndanda FC amesema neema ya ushamini na usajili wa wachezaji wenye umri mdogo
ndio vinawapa jeuri na kuamini hakuna kitakacho washinda, katika mapambano ya
kuwani ubingwa msimu huu.
Katika hatua nyingine Hamim Mawazo ametoa sababu
za Ndanda FC kushindwa kumsajili kiungo Athuman Iddy Chuji ambaye tayari alikua
ameshafanya makubaliano ya awali ya kuelekea mkoani Mtwara.
Post a Comment