SERIKALI MKOANI MBEYA YAUNDA KAMATI KWAAJILI YA KUCHUNGUZA AJALI ZA MOTO ZINAZOTOKEA MKOANI MBEYA
MBEYA
SERIKALI kupitia
mkuu wa wilaya ya mbeya
imeunda kamati maalumu kwa ajili
ya kufanya uchunguzi wa kina juu kuendelea kujitokeza
matukio ya kuungua kwa masoko
likiwemo soko la sido jijini mbeya.
Hatua hiyo inakuja
baada ya kujitokeza kwa ajari
ya moto kwenye soko hilo na
kuwasababishia hasara kubwa wafanya
biashara maeneo hayo.
Kufuatia kijitokeza
kwa ajari ya moto hususani kuungua
kwa masoko jijini mbeya kituo
hiki kimefanya mahojiano maalumu na
kamanda wa polisi mkoa mbeya Mohamad Mpinga
, amesema baada ya kupata taarifa jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya
ulinzi na usalama lilifika eneo la Soko la Sido ambalo lina wafanyabiashara
mbalimbali wanaouza vitu mbalimbali na kuanza jitihada za kuzima moto pamoja na
kuhakikisha usalama watu na mali zao.
Soko
hilo limeteketea kwa moto na mali zote zilizokuwa katika soko hilo
ambavyo bado thamani yake haijafahamika na kuwa Chanzo cha
moto huo bado hakijajulikana. Hakuna mtu/watu waliokamatwa kuhusiana na tukio
hilo. Hakuna madhara ya kibinadamu yaliyoripotiwa kutokea.
Aidha
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linatoa pole kwa wafanyabiashara waliopoteza mali
zao kutokana na janga hilo la moto na Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki
kigumu. Pia tunatoa shukurani kwa wananchi kwa ushirikiano mkubwa uliosaidia
kufanikisha kuzimwa moto huo ili usilete madhara makubwa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa
wito kwa wananchi kuepuka kukimbilia sehemu zenye majanga ya moto kwani ni
hatari kwa maisha yao na badala yake wajenge tabia ya kutoa taarifa mapema taarifa
kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuchukua hatua stahiki. Aidha
katika matukio kama hayo wananchi wajiepushe na uporaji wa mali za watu badala
yake wajikite katika uokoaji pekee.Hata hivyo hilo
ni tukio la tatu kutokea mkoani
mbeya , ambapo katika soko la sido
ni tukio la pili kutokea.
Post a Comment