WANANCHI WILAYANI KALAMBOMKOANI RUKWA WANUFAIKA NA MPANGO WA TASAF
ZAIDI ya
wananchi 4553 katika wilaya ya
kalambo mkoani Rukwa wamnenufaika
na mpango wa tasaf na
kuomba serikali kuongeza muda
wa utekelezaji ili
waweze kunufaika zaidi na
mpango huo .
Wameyasema hayo
kupitia mkutano wa hadhara uliokuwa
umeitishwa na mkuu
wa wilaya hiyo
Julith Binyura katika
kijiji cha Tatanda, ambapo wamepongeza mpango huo
na kuomba kuongezewa
fedha ambazo zitawasaidia kujikwamua
na hali ya
kiuchumi.
Mratibu
wa tasafu wilayani
humo ,maiko mwasumbi amesema
wanachi 4553 wamenufaika na
mpango huo na
kuwa licha ya
hilo mpango huo
umejikita zaidi katika kuwanufaisha wanafunzi
na watoto chini
ya umri wa miaka 5.
Mkuu wa wilaya
hiyo Julith Binyura, amewataka wanafaika
hao kuzitumia vizuri
fedha wanaopatiwa kwa
kuweka miradi ya
maendeleo .
Post a Comment