WANAFUNZI WAILILIA SERIKALI UHABA WA VYOO
MBOZI-SONGWE
Wanafunzi wa shule ya msigi
ichenjezya iliyopo katika halimashauri ya wilaya ya mbozi mkoani songwe
wameiomba serikali kuwasaidia kukamilisha ukalabati wa vyoo vya kisasa
vinavyojengwa shuleni hapo ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa matundu ya
vyoo tatizo ambalo limedumu kwa mda mrefu.
Wakizungumza na diratz news baadhi
ya wanafunzi wa shule hiyowamesema kuwa uhaba wa vyoo shuleni hapo unasababisha
athali kubwa na kuiomba selikari kuwasaidia kutatua changamoto hiyo kwani
kukamilika kwa vyoo hivyo wataepukana na foleni za chooni na kuepukana na
magongwa.
Afisa elimu shule za msingi sophia
shitindi amejibu kilio hicho cha wanafunzi na kusema miundo mbinu yote ya shule
ni jukumu la jamiii husika kuhakikisha wanaitengeneza ambapo amewataka
wanakijiji kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo.
Mwalimu mkuu shule ya msingi ichenjezya salvatory sikumbili |
Mwenyekiti wa shule ya msingi
ichenjezya badeni mwamarumbili amesema kuwa uhaba wa matundu ya vyo
inatokana na kutitia kwa matundu 10 ya yvoo lakini uongozi wa shule na kata
wanahakikisha wanatatua changamoto hiyo hata kwa kuanza na matundu 15 ya vyoo
ili kunusuru afya za wanafunzi.
Mkuu wa shule hiyo salvatory
sikumbili amesema kuwa shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 1300 na matundu ya
vyoo yaliyopo kwa sasa ni 8 matundu 4 kwa wasichana na 4 kwa wavulnahali
inayosababisha na wanfunzi kuwa watoro.
Post a Comment