DC KYELA AWATAHADHARISHA WANANCHI KUHAMA MABONDENI.
Kyela-Mbeya
SERIKALI Wilayani Kyela Mkoa wa Mbeya imewataka wananchi wanaoishi katika Meneo ya Mabondeni kuchukua tahadhari ili kuepekana na athari za Mafuriko zinazoweza kujitokeza kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha kipindi hiki cha mvua za masika.
Mkuu wa Wilaya Kyela, Claudia Kita alilieleza baraza la Madiwani la halmashauri ya wilaya hiyo hivi karibuni kuwa kuna uwekano wa kutokea maafa ya Mafuriko katika Maeneo ya Mabondeni kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo.
Alisema wananchi wanapaswa kuchukua hatua kwa kuhama katika maeneo hatarishi ambayo yanaweza kukumbwa na Mafuriko pamoja na kuzibua Mitaro ili kuruhusu maji kutiririsha maji kwa urahisi.
Kita alisema Wilaya ya Kyela ina Historia ya kukumbwa na Mafuriko mara kwa mara kutokana na hali ya kijiografia ilivyo hivyo inapofika wakati wa msimu wa mvua kila mtu anapasa kuchukua tahadhari ili kujiepusha na madhara ya Mafuriko.
“wakati mwingine maji ya mvua yanaweza yakawa yanatokea katika Wilaya jirani ya Rungwe au Ileje, ninawatake wananchi kuchukua hatua lakini na nyie madiwani mna jukumu la kuhimiza wananchi kuhama katika maeneo hayo, na sisi kama serikali tutahakikisha tunachukua hatua kukabiliana na janga hili,” alisema.
Katika hatua byingine Kita aliwaonya wananchi wanaofanya shughuli za kilimo na ufugaji pembezoni mwa mito kuacha mara moja kwani imekuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira katika Wilaya hiyo.
Alisema sheria inapiga marufuku wananchi kufanya shughuli zozote za binadamu ndani ya mita 60 kutoka kilipo chanzo cha maji na kinyume chake ni kinyume cha sheria za nchi.
Aliwaagiza madiwani kusimamia sheria za Mazingira katika maeneo yao kwani uharibifu umekuwa ukisababisha kina cha maji katika bandari ya Kyela kupungua kwa kasi hali inayotishia meli kushindwa kutia nanga katika bandari hiyo.
Madiwani katika halmashauri hiyo akiwemo,diwani wa kata ya Ikimba Katule Kingamkono alisema wamepokea agizo la Mkuu wa Wilaya na kwamba atahakikisha wanalitekeleza kikamilifu ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza.
Wilaya ya Kyela ipo eneo la bondeni hivyo wananchi wake wamekuwa wakiathirika kila mwaka kipindi cha mvua za mafuriko kutokana na maji yatokayo kwenye mito inayoanzia wilaya ya Rungwe iliyopo kwenye muinuka hutiririsha kuelekea Kyela na kusababisha maafua kila msimu.
Post a Comment