Header Ads


WADAU MBALIMBALI WAOMBWA KUWEKEZA KATIKA HIFADHI YA KITULO


Mhifadhi msimamizi katika Hifadhi ya Kitulo,Eva Pwele alibainisha hayo alipozungumza na wachama wa Chama cha waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji nchini(TAJATI) waliofanya ziara ya siku moja hifadhini hapo.

Pwele alisema bado hifadhi inakabiliwa na changamoto kubwa ya kukosekana kwa nyumba ya kulala watalii hatua ambayo husababisha baadhi yao kupelekwa kijiji jirani cha Matambo ili wakalale.

Hata hivyo Pwele alisema hatua ya kulala nje ya hifadhi imekuwa ikionekana kutowapendeza watalii wengi kwani mara nyingi wanahitaji kuwepo katika mandhari mazuri ya hifadhi hiyo wakati wote.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TAJATI,Ulimboka Mwakilili alisema kuna haja ya watanzania kuchangamkia fursa za uwekezaji ndani ya hifadhi ya Kitulo kutokana na dalili nyingi za kuwepo ongezeko la watalii siku za usoni kutokana na vivutio lukuki vilivyopo.


Mwakilili alisema vivutio kama Ndege wanaosafiri kutoka Kaskazini mwa bara la Ulaya na kutua hifadhini hapo kwa mapumziko kabla ya kuelekea Afrika kusini,maporomoko mengi ya maji na maua ya aina mbalimbali vikiendelea kutangazwa kwa kasi kutawezesha watalii wengi kufika.

Naye makamu mwenyekiti wa chama hicho,Christophe Nyenyembe alisema uwekezaji wa michezo ya Gofu na,Mbio za baiskeli na Farasi pia unaweza kuwa kivutio kingine kwa watalii.

No comments

Powered by Blogger.