Header Ads


MKUU WA MKOA WA MBEYA AMOSI MAKALA AWATAKA WANAFUNZI WA KIKE KUDANGANYWA

MBARALI-MBEYA
WANAFUNZI wa Kike mashuleni wametakiwa kuepukana na Ahadi za kuonana baadaye kwakuwa kufanya hivyo kunaweza pia kuwasababishi kushindwa kufikia malengo yao ya baadaye.

Mkuu wa  mkoa wa Mbeya,Amos Makalla alipiga marufuku ahadi hizo aliupokuwa akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Madibira iliyopo katika kata ya Madibira wilayani Mbarali.

Makalla alisema kuna tabia iliyojengeka kwa wanafunzi wa vidato vya juu kuwarubuni waliopo vidato vya chini na kuwashawishi kuanzisha mahusiano ya kimapenzi kwa madai kuwa watawaoa baada ya kumaliza shule.

“Wapo wanafunzi wa kiume ambao kwa kuwa wapo kidato cha nne au cha sita wanaanza kuwadanganya mabinti walioko vidato vya chini..Ooooh unajua mimi ntatangulia kumaliza shule…kwahiyo usijali utakuta mimi nimeshakuandalia maisha hivyo nitakuoa.Hakuna kitu kama hicho na kuanzia leo usikubali ahadi ya namna hiyo”

“Muhimu ni kuzingatika kilichokuleta hapa shuleni.Malengo yako ya kuwa hapa ni nini? Haukuja kutafuta mchumba hapa ulikuja kusoma ili baadaye ufikie malengo yako. Hapa tuna wanasiasa na wataalamu mbalimbali sasa usikubali ndoto yako kufutika kwa ahadi ya kukuoa”alisisitiza Makalla.

Mkuu huyo wa mkoa pia alitoa muda wa wiki mbili kwa Halmashauri ya wilaya ya Mbarali na Tanesco  kuhakikisha wanatatua changamoto ya kutopatikana kwa maji shuleni hapo kutokana na kutokana na kutofungwa kwa mashine ya kusukuma maji.

Alisema kutopatikana kwa maji safi na salama shuleni hapo kunahatarisha afya ya wanafunzi na walimu na pia kunasababisha changamoto ya kutumia muda mwingi kuyafuata maeneo ya mbali.

No comments

Powered by Blogger.