Header Ads


BILIONI 59.753 ZINATARAJIA KUTUMIKA KWENYE MRADI WA BARABARA CHUNYA

CHUNYA-MBEYA
SHILINGI Bilioni 59.753 zinatarajiwa kutumika katika mradi ya ujenzi wa baraba ya Chunya hadi Makongorosi chenye urefu wa kilomita 39 kwa kiwango cha lami na kuondoa adha ya usafiri katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara(Tanroads) mkoa wa Mbeya,Eliazary Rweikiza mradi huo unagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 na unatekelezwa na Kampuni ya China Railway 15 bureau Group Corparation.

Rweikiza alisema mradi huo unasimamiwa na Kampuni ya Mhandisi  Mshauri SMEC Inernational Pty Limited kwa kushirikiana na  kampuni ya Mhandisi Consultancy kwa gharama ya shilingi  2,651,640,658.

Alisema hadi sasa mkandarasi aliyeanza kazi tangu Oktoba mwaka jana amelipwa shilingi bilioni9 2.241 sawa na asilimia 25 na kiasi hicho ni sawa na asilimia 3.7 ya fedha ya mkataba.

Kaimu meneja huyo alisema mradi huo utatekelezwa kwa  miezi 27 hivyo unatarajiwa kukamilika  mwaka 2020 ambapo kwa sasa kazi zinazoendelea ni pamoja na ujenzi wa kampi na kuwasilisha vifaa kwenye eneo la kazi.

“Kipande hiki ni sehemu ya barabara ya Mbeya-Rungwa yenye urefu wa kilomita 293 inayoungania mkoa wa Mbeya na mikoa jirani ya Tabora na Singida.Serikali imekuwa ikijenga barabara hii kwa kiwango cha lami kwa awamu.Awamu ya kwanza nay a pili kutoka jijini Mbeya hadi Chunya kilometa 72 imekwishakamilika.”alisema Rweikiza

No comments

Powered by Blogger.