DC KYELA AWAPA SOMO WALIOHITIMU KIDATO CHA NNE,AWATAKA KUTOJIINGIZA KWENYE NDOA.
Mkuu wa Wilaya ya Kyela Bi.Claudia Kitta |
KYELA-MBEYA
MKUU wa Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya Claudia Kitta, amewataka
wanafunzi ambao hawajachaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza mwaka huu
kuachana na Fikra za kutaka kuoa au kuolewa na badala yake wafikirie
kujiunga na elimu ya ufundi stadi ili wajikwamue kiuchumi.
Kita ametoa rai hiyo jana wakati akizungumza na Madiwani wa
halmashauri ya Wilaya ya Kyela walipokuwa kwenye kikao cha kujadili na kupitia
taarifa za kamati mbalimbali katika kipindi cha robo mwaka fedha 2017/2018.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema Jumla ya wanafunzi 2710 kati ya
7338 waliofanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi hawajabahatika kuchaguliwa
kujiunga na Kidato cha kwanza kutokana na kufanya Vibaya.
Alisema Idadi hiyo ya wanafunzi waliosalia nyumbani ni kubwa
hivyo wazazi na walezi wana wajibu wa kuhakikisha wanawapeleka kwenye shule
binafsi au shule za ufundi ili wawezi kupata ujuzi wa kufanya kazi za
Mikono utakaofanya waweze kujitegemea hapo baadae.
“kwa takwimu nilizonazo wanafunzi 2710 hawajachaguliwa
kujiunga na Kidato cha kwanza mwaka huu hao wapo nyumbani, nitoe rai kwa wazazi
na walezi tusiwaacha tuwapeleke shule za ufundi wakajifunze kazi za mikono, pia
wao waachanae na fikra za kuoa au kuolewa kwa kuwa bado wana umri mdogo,”
“Pia na nyie Madiwani mtusaidie katika hili nah ii itasaidia
hata vijana wetu ambao wapo nyumbani kutojiingiza kwenye Makundi Mabaya ikiwemo
Madawa ya Kulevya na uhalifu mwingine kwa kisingizio cha ukosefu wa ajira,”
alisema.
Aidha, Mkuu huyo wa wa wilaya aliwataka wananchi wa wilaya
hiyo kuendelea na kilimo katika msimu huu na kuwahakikishia kuwa Mbolea aina
ya UREA ipo ya kutosha isipokuwa bei imeongezeka kidogo kutokana na
gharama za manunuzi na usafirishaji.
Hata hivyo hakuweka bayana gharama ya sasa ya Mbolea hiyo
kwa madai kuwa hadi kamati ya Pembejeo ya wilaya itakapoketi kupitia mchakato
mzima wa usambazaji na kusisitiza kuwa inapatikana kwa bei ambayo kila mkulima
anaweza kuimudu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya hiyo
Hunter Mwakifuna aliwataka Madiwani na wananchi kutotafsri vibaya kauli
ya rais John Magufuli ya kupiga marufuku michango shuleni.
Alisema Kauli ya raisi inawapiga marufuku walimu na maafisa
elimu kuwatoza michango wazazi na walezi na kwamba wananchi wanaweza kuamua
kuchangia michango mbalimbali ikiwemo chakula kwa kibali kutoka kwa mkurugenzi
wa halmashauri.
Post a Comment