CDF YADHAMIRIA HAYA KWA JESHI LA POLISI
DAR ES SALAAM
KAMISHNA
msaidizi wa Polisi (SACP) ambae pia ni Mkuu wa idara ya Rasilimali watu
Jeshi la Polisi Makao Makuu Benedict Wakulyamba, amewataka maofisa wa
Jeshi la Polisi waliopata mafunzo ya ushauri Nasihi kufanya kazi kwa
uadilifu ili kuweza kuisaidia jamii kutokana na changamoto
zinazowakabili.
Akizungumza na maofisa hao mapema leo hii,Jijini Dar es Salaam alipokua
akifunga mafunzo ya siku tano yaliodhaminiwa na Shirika la utu wa mtoto
(CDF), ambayo yamelenga kupambana na ukatili wa kijinsia hususani
upande wa wanawake na watoto amesema endapo watayatumia vizuri mafunzo
hayo basi watafanikiwa kwa kiwango kikubwa.
"Nyinyi mmeaminiwa kuenda kujua matatizo ya watu,Changamoto za watu
ndani ya jamii kutokana na nyazifa zenu na maadili ya kazi yenu hivyo ni
vyema mukaenda kutenda kazi zenu kwa uadilifu mkubwa ili kuleta
mabadiliko juu ya suala hili, kwani changamoto hizi hazipo katika jeshi
la polisi tyu hata uraiani zipo "amesema kamishna Wakulyamba.
Aidha ameongeza kuwa,licha ya kuwa baadhi ya mikoa hawakufika katika
mafunzo hayo, lakini watahakikisha kila Wilaya anakuepo mtu wa kuweza
kutoa ushauri Nasihi na ikibidi kila kituo awepo ili kuweza kukabiliana
na changamoto za ukatili wa kijinsia.
Kwa upande wake,Meneja Mipango wa Shirika hilo, Dorothy Ernest amesema
kuwa Tatizo la ukatili wa kijinsia lipo kwa kiwango kikubwa hususani
upande wa wanawake na watoto ndio maana wakaamua kudhamini mafunzo hayo
na kufanya kazi kwa karibu na Jeshi la Polisi ili kuweza kuwapatia
msaada wahanga wa tatizo hilo.
"Tumeamua kufanya kazi na Jeshi la Polisi kwa karibu zaidi kutokana na
kupokea wahanga wengi wa tatizo hili, na tunakuwa tunawaelekeza kwenu
ili muweze kuwapa msaada, sasa kama hujapata mafunzo haya inakuwa ni
ngumu kuweza kumpa msaada"amesema Dorothy.
Aidha amesema, mafunzo hayo yamelenga kuimarisha madawati ya kijinsia
nchi nzima na kuziba mapengo yote, na kusisistiza kuwa wataendelea
kufanya kazi kwa karibu na Jeshi la Polisi ili kuhakisha wanapunguza
tatizo hilo kwa kiwango kikubwa .
Post a Comment