Header Ads


KAMBI YA RIADHA YA DUNIA YA PAMBA MOTO MWINGINE ACHAGULIWA KUJIUNGA LONDON


Dar es Salaam.
 Hatimaye kikosi cha timu ya Taifa ya riadha kitakachoshiriki mashindano ya dunia kimeingia kambini Arusha, huku idadi wanariadha ikiongezeka baada ya mwanariadha, Failuna Abdi kufikia viwango.
Kocha wa timu hiyo, Zacharia Barie amesema tayari wanariadha sita wako kambini katika misitu ya Mura huko Arusha.

"Wanariadha wote waliofikia viwango isipokuwa Fabiano Joseph wameingia kambini, Failuna pia tunamtegemea kujiunga na wenzake keshokutwa (Alhamisi)," alisema Barie.
Failuna amefuzu katika mbio za Diamond League zilizofanyika wikiendi iliyopita huko Uholanzi akitumia dakika 31:47:31 kumaliza mbio za mita 10,000 muda uliomuwezesha kufikia viwango vya kushiriki mashindano ya dunia.
Wanariadhawengine waliofuzu ni Said Makula, Alphonce Simbu, Jafar Juma, Sarah Ramadhan, Magdalena Shauri watakimbia mbio za marathoni, huku Gabriel Geway atakimbia mbio za mita 10,000.

No comments

Powered by Blogger.