NYOTA WAZAMANI WA YANGA AUNGANA NA WENZAKE KUMPIGIA DEBE MAYAY URAISI TFF
DAR ES SALAAM
Kocha Adolph Rishard amesema anamuunga mkono Ally Mayay aliyechukua fomu ya kugombea urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwani anatosha katika nafasi hiyo.
Mayay
amerudisha fomu leo za kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa TFF
utakaofanyika Agosti 12 akichuana na Jamal Malinzi, Athumani Nyamlani,
Frederick Mwakalebela, Imani Madega, Wallace Karia na Fredrick Masolwa.
Rishard
alisema yeye pamoja na wachezaji wa zamani wanamuunga mkono Mayay na
wanaamini akipata nafasi hiyo ataliongoza vema shirikisho hilo na
kuupeleka mbele mpira wa Tanzania.
Alisema hawamuungi
mkono Mayay kwa kuwa alicheza mpira zamani bali ana sifa zote za
uongozi na ndio maana wameona anatosha katika nafasi hiyo.
"Siyo kama anafaa kuiongoza TFF kwa sababu amecheza mpira, hapana ila ana uwezo mkubwa wa uongozi na ana nidhamu.
"Ana
elimu, amewahi kupata uongozi katika sehemu mbalimbali kama chuo, Yanga
na kwingineko hivyo kwa uzoefu wake alioupata huko tumeona kuwa anafaa
pia kuongoza hata TFF," alisema Rishard.
Alisema pia Mayay analijua soka vizuri kwani licha ya kucheza kipindi cha nyuma, pia ni mchambuzi wa soka.
Katika
nafasi ya makamu wa rais waliochukua fomu mpaka sasa Mulamu Nghambi,
Michael Wambura, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ na Mtemi Ramadhan.
Post a Comment