SHULE WENYE MAHITAJI MAALUMU KUJENGWA PATANDI
DODOMA
Mpango huo umebainishwa leo (Jumanne) bungeni na Waziri wa Elimu,
Profesa Joyce Ndalichako alipokuwa akitoa mchango wa mwisho wa makadirio
ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18.
"Licha ya kuwapa nafasi ya mafunzo walimu hao, shule hiyo itasaidia
kukidhi mahitaji ya wenye uhitaji," amesema Waziri Ndalichako.
Amesema kutatua kero za wanafunzi wenye mahitaji maalumu ni kipaumbele
cha wizara yake. Hilo, amesema, linatekelezwa sambamba na usimamizi wa
ubora wa elimu nchini.
"Tumetenga fedha za kujenga ofisi 50 za wakaguzi pamoja na kuongeza
rasilimali watu," amesema.
Kuanzia mwaka ujao wa fedha, amesema wizara itaondoa tofauti iliyopo
kati ya wakaguzi wa shule za msingi na sekondari.
"Utaratibu huo umepitwa na wakati. Kwa sasa, kila ilipo shule ya msingi
kuna sekondari pia," alieleza.
Post a Comment