Header Ads


SINGIDA UTD HAINA MPANGO WA KUWASAJILI WACHEZAJI WATOKAO TIMU ZA SIMBA,YANGA NA AZAM


Arusha.
Kama unadhani Singida United inawatolea macho wachezaji Simba na Yanga, utakuwa umekosea kwani uongozi wa timu hiyo wamesema hawana mpango wa kuwasajili wachezaji kutoka klabu hizo mbili.
Mkurugenzi wa Singida United, Yusuph Mwandani amesema kamati yao ya usajili imezipa kisogo kabisa wachezaji waliochezea Simba, Yanga au Azam kutokana na wengi kutokuwa na viwango vikubwa uwanjani zaidi ya kuchezea majina yao makubwa (umaarufu)

“Wachezaji waliochezea Simba na Yanga hasa msimu huu hakuna wa kututamanisha kuipata saini yake… kwanza hatuwapendi maana wengi hawana viwango vya uwanjani vile tunavyotaka bali wengi ni umaarufu tu unawafanya kugombewa hivyo ujio wetu usizitishe klabu hizi zikidhani tutawagombea wachezaji wao”
Alisema Singida United inataka wachezaji wazuri wa uwanjani watakaoweza kuifikisha timu hiyo katika malengo ya kutwaa ubingwa wa soka Tanzania bara.
Alisema kuwa msimu ujao wanataka kuuonyesha mapinduzi wa kisoka katika Ligi Kuu kwa kutwaa ubingwa na kumaliza utawala wa Dar es Salaam kunyakuwa taji hilo mara kwa mara.

No comments

Powered by Blogger.