WAZIRI WA AFYA NA USTAWI UMMY MWALIMU AMECHUKIZWA NA KITENDO CHA HOSPITALI TEULE YA WILAYA MJINI NAMANYERE NDDH KWA KUSHINDWA KUFUATA KANUNI
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Waziri Ummy Mwalimu |
NAMANYERE-RUKWA
WAZIRI wa afya na ustawi Ummy
Mwalimu amechukizwa na kitendo cha Hospitali teule ya wilaya mjini Namanyere
NDDH kwa kushindwa kufuata kanuni za mkataba uliopo kati yao na serikali na
kuitaka halmashauri ya wilaya Nkasi kupitia madiwani kuchukua hatua kama hari
hiyo itaendelea.
Akizungumza mara baada ya kupokea
taarifa ya mkoa Rukwa iliyosomwa na mganga mkuu wa mkoa Rukwa Dkt,Boniface
Kasululu ikulu ndogo wilayani Nkasi alisema kuwa amepata taarifa za kiutendaji
zisizoridhisha katika hospitali hiyo teule na kuvunja mikataba waliyowekeana na
serikali kitu ambacho ni kinyume chas sheria.
Amesema serikali inapeleka fedha
nyingi katika hospitali hiyo sambamba na watumishi kadhaa wa serikali lakini
taarifa alizonazo zimemvunja moyo na kuwapa jukumu madiwani kufuatilia ikiwa ni
pamoja na kuchukua hatua.
Waziri Ummy amefafanua kuwa kwa sasa
mikataba yote ya namna hiyo itakuwa inafanywa na madiwani ili wawe na uwezo wa
kuchukua hatua stahiki pale mambo yanapokwenda kinyume na mkataba waliowekeana.
Sambamba na hilo amezitaka
halmashauri zote mkoani Rukwa kujenga hospitali zao za wilaya na kuwa mpango
uliopo sasa ni halmashauri zote Nne zilizopo mkoani Rukwa kuhakikisha kuwa
wanajenga hospitali za serikali za wilaya na kuwa hilo ndiyo litakuwa suluhisho
la changamoto hizo wanazokumbana nazo kwenye ubia na hospitali za mashirika.
Katika hatua nyingine Waziri huyo wa
afya aliupongeza mkoa Rukwa kwa kufanikiwa kupunguza vifo vya kina Mama
wajawazito kwa 95% na wajawazito wengi kuweza kujifungulia kwenye vituop vya
kutolea huduma.
Amesema mpango wa serikali sasa ni
kutaka kupunguza vifo vya kina mama wajawazito kwa asilimia kubwa na kuwa mkoa
Rukwa umeonyesha njia ya kuweza kufanikiwa juu ya hilo na kuwa mkoa Rukwa una
idadi ndogo ya watumishi wa afya lakini wamefanikiwa katika hilo na kuahidi
kuwa katika ajira mpya watahakikisha wengi wa watumishi hao wanapelekwa mkoani
Rukwa ili kuweza lkurahisha huduma hizo kwa Wananchi.
Post a Comment